.jpg)
Viongozi
wa Mkoa wa Kigoma wakiwa katika eneo la ajali wakiangalia zoezi la
upoaji wa miili iliyopatikana katika ziwa Tanganyika kufuatia ajali ya
mitumbwi iliyotokea jana. Nao ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Mstaafu
Issa Machibya (wa pili kushoto) anayefuata ni Katibu Tawala wa Mkoa John
Nduguru na Ramadhani Maneno Mkuu wa Wilaya ya Kigoma. Kushoto ni
Mwenyekiti wa CCM wa Kigoma
.jpg)
Waokoaji wakiwa wamebeba mwili uliopatikana katika ziwa Tanganyika baada ya ajali ya mitumbwi katika kijiji cha kalalangabo
.jpg)
Wanajeshi
wa Jeshi la Wananch (JWTZ) wakiendelea na zoezi la kuopoa miili ya watu
waliopata ajali ya mitumbwi katika kijiji cha Kalalangabo baada ya
mitumbwi waliyokuwa wakisafiria kuzama
.jpg)
Zoezi
la uopoaji wa miili linaendelea na vikosi mbalimbali vya ukoaji katika
ziwa Tanganyika kufuatia ajali ya mitumbwi iliyotokea jana
Na Editha Karlo wa Globu ya jamii Kigoma
Mpaka
sasa jumla ya maiti nne zimeopolewa na kufanya kufikia idadi ya maiti
kumi zimepatikana katika ajali ya mitumbwi iliyotokea jana mchana katika
kijiji cha Kalalangabo baada ya mitumbwi iliyokuwa imebeba maharusi
ndugu jamaa na wapambe kupigwa wimbi na kuzama.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma Luteni Mstaafu Issa Machibya ambaye ni Mwenyekiti wa
kamati ya maafa ya Mkoa amesema kuwa bado idadi maiti zilipo kwenye maji
ni kubwa ambazo bado hazijapatikana.
''Zoezi
hili linakuwa gumu sababu ya uhaba wa waokoaji pamoja na miundombinu
duni ambavyo ni kikwazo katika zoezi hili la ukoaji. Lakini bado
tunaendelea na kazi ''Mkuu wa Mkoa huyo ameiambia Globu ya Jamii asubuhi
hii.
No comments:
Post a Comment