Prizenta wa Star TV, Sauda Mwilima akiwa na mume wake, Kauli Jumasiku ya harusi yao.
Oooh nooo! Miaka
miwili baada ya kufunga pingu za maisha (ndoa) na mwanaume aitwaye
Kauli Juma, imefichuka kwamba ndoa ya prizenta wa Star TV, Sauda Mwilima
ina shida kwani haishi na mumewe, ikidaiwa kwamba kila mmoja anaishi
nchi tofauti na mwenzake.

Kikizungumza na paparazi, chanzo makini
ambacho ni mtu wa karibu wa Sauda, kilisema kwamba baada ya wawili hao
kufunga ndoa, Kauli aliondoka kwenda nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’
alikokuwa akifanya shughuli zake kabla ya kufunga ndoa na hadi leo
hajawahi kurudi Tanzania.
“Yaani baada ya Sauda kufunga ndoa,
mumewe alikaa kwa miezi michache hapa Bongo, nasikia hata tendo la ndoa
walifanya mara mbili tu.
“Hata alipojifungua na mtoto kufariki
dunia kwa bahati mbaya, mumewe hakuwepo na hadi leo hajarudi, ukweli
inauma sana ila Sauda ni mvumilivu kwani ndoa yake ni shida,” kilisema
chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi alimtafuta Sauda ambapo alikuwa na haya ya kusema:
Sauda Mwilima akivishwa pete na mume wake, Kauli Juma.
“Ni kweli anaishi Sauzi. Tangu tukiwa
wachumba tulielewana kwamba tukioana kila mtu ataendelea kuishi
anapoishi hivyo mume wangu anafanya shughuli zake nchini Afrika Kusini
na huwa anakuja mara mojamoja akiwa na nafasi au akiwa likizo.
“Mimi siyo mtu wa kujionesha kwamba eti
mume wangu yupo nchini hivyo akija huwa ni kimyakimya anakaa tunaendelea
na mambo ya familia yetu basi muda ukiisha anaondoka na tulikubaliana
tangu tukiwa wachumba hivyo ikitokea mmoja wetu ameamua kumfuata
mwenzake na kwenda kuishi naye hakuna shida,” alisema Sauda.
Sauda aliongeza kwamba ndoa yake iko vizuri na hawajaachana na endapo ingekuwa haipo asingevaa pete ya ndoa.
“Ndoa yangu haijavunjika, tuko vizuri na mume wangu japokuwa tuko mbali lakini kila mmoja anamwamini mwenzake,” alisema Sauda.
Wadau wanaifananisha ndoa hiyo na ya Aunt Ezekiel na kudai kuwa wawili hao hawachekani.
No comments:
Post a Comment