Acha kabisa! Habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa wa Kibongo ni madai ya Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuwachanganya kimalovee, mastaa wenzake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Vanessa Mdee ‘Van V’ au V-Money.
Akizungumza na paparazi namba moja kwa
habari za mastaa Bongo, chanzo makini kilisema Jokate na Vanesa kwa sasa
ni kama chui na paka kufuatia hivi karibuni Jokate kudaiwa kuingilia
penzi la mwanzake na mpaka sasa eti ndiye aliyeshikilia usukani.
“Sasa hivi Jokate na Ommy ni mahaba niue kwani mara nyingi wanakuwa pamoja.
“Hadi Jokate anakwenda geto kwa Ommy jambo ambalo limesababisha yeye na V-Money kutoelewana kwani awali ndiye alikuwa kiburudisho cha Ommy,” kilidai chanzo hicho.
“Hadi Jokate anakwenda geto kwa Ommy jambo ambalo limesababisha yeye na V-Money kutoelewana kwani awali ndiye alikuwa kiburudisho cha Ommy,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizi, paparazi alimtafuta mhusika mkuu Ommy Dimpoz ambaye alikuwa na haya ya kusema:
“Ehee! Ndiyo nasikia kwako, kwani
wasanii haturuhusiwi kupendana jamani, hata Mwalimu Nyerere (Baba wa
Taifa) alisema tuwe pamoja kwa hiyo Jokate ni rafiki yangu wa karibu na
huyo Vanessa sijawahi kuwa na uhusiano naye but (lakini) alikuwa
mshikaji tu.”
Juhudi za kuwapata Jokate na Vanessa
ziligonga mwamba baada ya simu zao kuita bila kupokelewa hivyo jitihada
zinaendelea ili kila mmoja aeleze la moyoni mwake.Juzikati picha za
Jokate na Ommy wakiwa kimahaba zilizagaa kwenye mitandao mbalimbali hali
iliyozua viulizo kibao kwa mashabiki wao.
No comments:
Post a Comment