Mwanafunzi wa Chuo cha Uuguzi Chimala wilayani
Mbarali, Mkoa wa Mbeya, Vena Mtati (27) (pichani) anashikiliwa na Jeshi
la Polisi Mkoa wa Iringa kwa madai mazito ya kumuua mtoto wake kwa
kumnyonga, kumtumbukiza kwenye mfuko wa rambo na kuutia ndani ya mfuko
wa salfeti kisha kuuficha chini ya kitanda.
Tukio hilo la kikatili ambalo limewashangaza wengi, hasa ikizingatiwa
kuwa mtuhumiwa huyo anajua sheria kwa sababu anajifunza uuguzi,
lilijiri Agosti 21, mwaka huu ndani ya nyumba moja iliyopo Kijiweni,
Kata ya Mvinjeni mjini hapa.

Kwa mujibu wa shuhuda ambaye anaishi
jirani na nyumba inayodaiwa kufanyika mauaji hayo (jina lipo), wiki
mbili zilizopita, mtuhumiwa huyo alifika kwenye nyumba hiyo akitokea
chuoni akiwa na ujauzito.

“Wiki mbili zilizopita, Vena alifikia kwa rafiki yake anayeitwa Joyce
ambaye alikuwa amepangisha katika hiyo nyumba. Vena alikuwa na mimba
kubwa, baada ya siku tano tu akajifungua,” kilisema chanzo hicho.

Kikaongeza: “Siku ya tukio, Joyce yeye ambaye ni mwenyeji alitoka
kwenda katika shughuli zake, akamuacha Vena akiwa chumbani. Nadhani
ndipo aliposhikwa na uchungu, akajifugua mtoto wa kike.

“Ilikuwa
asubuhi, sisi tukasikia kelele kutoka kwenye chumba hicho. Zile kelele
zilikuwa si za kawaida! Ilikuwa kama vile kuna mtu anakabwa.

“Tuliposikiliza kwa makini, mara sauti ya redio ikaongezwa ili
kufanya kelele hizo zisisikike kwa nje. Lakini kwa vile sisi majirani
tulijua kwamba ndani ya chumba kile kuna mjamzito na kelele alizopiga
mtoto si za kawaida ndipo tulipomtafuta mwandishi wa habari (hizi),”
kilisema chanzo hicho.

Mwandishi wetu alipopatikana na
kunyetishiwa kuhusu kuwepo kwa uwezekano wa mama ambaye ni nesi kumuua
mtoto wake aliyejifungua, aliwasiliana na Polisi wa Dawati la Jinsia.

Denti (aliyeshika kiroba chenye mwili) akiwa chini ya ulinzi wa polisi (Kulia) ni mwenyeji wake, Joyce.
Polisi hao, awali walimtafuta mwenyeji wa mtuhumiwa huyo, yaani Joyce
ambaye alikuwa kwenye mihangaiko yake.
Alipopatikana alipokonywa simu
yake ya mkononi ili asiweze kuwasiliana na mtuhumiwa.

Aliulizwa kama ana mgeni nyumbani kwake, akakiri. Akaulizwa kama
mgeni huyo amejifungua, akakataa ndipo wakamchukua kwenda naye nyumbani
kwake kumfuata mtuhumiwa huyo.

Mwandishi wetu akiwa ameongozana na askari hao walifika kwenye chumba hicho na kumkuta Vena akiwa amesimama mlangoni.
Alipoulizwa kama amejifungua, awali alikataa katakata lakini baada
ya kubanwa na kutishiwa kuswekwa ndani, alikiri kujifungua na kusema
kwamba mtoto huyo amemficha uvunguni mwa kitanda.

Ndani ya chumba hicho, sakafuni kulikuwa na damu zilizodaiwa kumtoka mtuhumiwa huyo wakati akijifungua mwenyewe!
Polisi walizama
chumbani, wakainama kuchungulia chini ya kitanda. Walichoanza kukiona ni
mfuko wa salfeti, wakauvuta kuutoa. Walipofungua ndani, wakakuta mfuko
wa rambo, wakaingiza mkono na kutoa kifurushi kikiwa kimeviringishwa
nguo nyingi na ndiye mtoto huyo alimohifadhiwa.

Mbali na mwili wa
mtoto huyo kuviringishwa nguo hizo, pia ulimwagiwa chumvi na vumbi la
mkaa ambapo ilidaiwa mtuhumiwa alifanya hivyo ili mwili huo usitoe
harufu utakapotupwa porini.

Majirani walisema maarifa hayo, mtuhumiwa aliyapata kwa sababu tayari
anajua namna ya kuhifadhi mwili wa mwanadamu, kwa mwanamke asiye na
ujuzi asingeweza kufanya hivyo.

Kuna madai kwamba,
mtuhumiwa huyo aliwaambia polisi kuwa alifikia uamuzi wa kumuua mtoto
huyo kufuatia mwanaume aliyempa ujauzito aishiye jijini Dar es Salaam
kumuahidi ndoa lakini akaingia mitini.

Baada ya polisi
kusikiliza maelezo ya mtuhumiwa huyo, walimkamata yeye, mwenyeji wake
Joyce na mmiliki wa nyumba hiyo ambaye jina halikupatikana mara moja.

Polisi walisema mmiliki wa nyumba hiyo alikamatwa kwa sababu alikiuka
sheria za mji ambapo alitakiwa kutoa taarifa za kumpokea mgeni huyo
kwenye serikali za mitaa lakini hakufanya hivyo huku Joyce akidaiwa
kutambua kuwa mgeni wake alijifungua lakini akawaambia hakujifungua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

No comments:
Post a Comment