JINI KABULA ANASWA MTUMBANI AKINUNUA NGUO
WAKATI mastaa
hupendelea kufanya shopping katika maduka makubwa, msanii wa filamu
Miriam Jolwa maarufu kama Jini Kabula, mwishoni mwa wiki iliyopita
alinaswa akichagua gauni alilodai ni la harusi katika duka la mitumba
lililopo Makumbusho jijini Dar.
Msanii wa filamu, Miriam Jolwa maarufu kama Jini Kabula akiwa na rafiki yake Isabela wakifanya shopping katika duka la mitumba.
Msanii huyo akiwa na rafiki yake, Isabela walikutwa wakiwa bize katika duka hilo linalofahamika kama kwa Mzee wa Pamba.
“Kwani kuna ajabu gani mimi kuja kununua
gauni la harusi yangu mtumbani? Watu wanashidwa kuelewa kuwa magauni ya
mitumba ni mazuri sana” alisema baada ya kuulizwa kulikoni asiende
kwenye maduka makubwa ya nguo.
3:44 PM
No comments:
Post a Comment