BAADA ya kushikiliwa kwa takriban miezi tisa kwa kesi ya madawa ya kulevya ‘unga’, hatimaye Video Queen maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela huku kukiwa na uwezekano wa kupunguziwa adhabu ikawa ndogo zaidi
HUKUMU NYEPESI? Kwa
mujibu wa mtu wa karibu wa Jack, modo huyo alihukumiwa Jumatatu
iliyopita (Agosti 11, mwaka huu) kwenye Mahakama ya Macau huko Hong Kong
ambapo hukumu hiyo ilitofautiana na adhabu nyingine za madawa nchini
humo ambazo huwa hukumu yake ni kunyongwa hivyo ya Jack kuonekana
nyepesiii! KWA NINI NYEPESI?
Kikimwaga data, chanzo hicho makini
kilidai kwamba, hukumu hiyo ya Jack ni nyepesi ukilinganisha na hukumu
nyingine za madawa ya kulevya zinazotolewa nchini China ambapo hakimu
alitumia muda wa dakika 27 tu kuisoma.
“Hukumu za madawa ya kulevya
zinatofautiana nchini China. Kuna baadhi ya majimbo kama Beijing huwa
wao ikithibitika umebeba madawa ya kulevya, unanyongwa lakini baadhi ya
maeneo unafungwa miaka kadhaa. Miaka hutofautiana kulingana na sheria
walizojiwekea,”
kilifunguka chanzo chetu. HUKUMU YA JACK
IPOJE? Ilidaiwa kwamba, kwa mujibu wa hukumu hiyo aliyohukumiwa mrembo
huyo, anaweza kupunguziwa muda wa kifungo kulingana na nidhamu
atakayoionesha gerezani kama mahakama ilivyoelekeza.
“Anaweza akapunguziwa kifungo kwa sababu
hukumu imeeleza wazi kwamba anaweza kupunguziwa adhabu hiyo kama
atatimiza masharti ya kinidhamu ambayo sheria za China zinamtaka
atimize,” kilisema chanzo hicho.
TUJIUNGE NA CHANZO “Amehukumiwa juzi
Jumatatu, ametakiwa kwenda jela miaka sita, nilikuwa nikiwasiliana naye
mara kwa mara lakini juzi hiyo ndiyo kanitumia taarifa kwamba
amehukumiwa na kunieleza kwamba siku hiyo aliduwaa kwa muda maana
hakuamini kama anaweza kuhukumiwa kwani alikaa muda mrefu bila kujua
hatima yake,” kilisema chanzo hicho kilicho karibu na Jack.
JACK AFURAHIA HUKUMU! Chanzo hicho
kilizidi kumwaga data kuwa, baada ya hukumu hiyo kupitishwa, Jack
alifurahia hususan kuwepo kwa kipengele cha uwezekano wa kupunguziwa
kifungo kama atakidhi masharti aliyopewa na mahakama.
“Baada ya kutafakari kwa kina hukumu
yake, Jack anaonekana kuifurahia kwa sababu anaamini kwake yeye itakuwa
ni rahisi kutimiza masharti ya kuwa mstaarabu kadiri kipengele hicho
kilivyomuelekeza,” kilisema chanzo. NDUGU HAWAJUI LOLOTE? Katika hatua
nyingine, chanzo hicho kilifunguka kuwa ndugu wa Jack waliopo Bongo
hawakuwa na taarifa zozote kuhusiana na hukumu hiyo.
Kilisema kuwa kwa upande wake
iliwezekana kupata haraka taarifa hizo kwani alikuwa akiwasiliana na
Jack mara kwa mara kwa njia ya barua. “Ilikuwa ni rahisi mimi kunipa
taarifa hizi haraka kwa sababu nilikuwa nikiwasiliana naye mara kwa
mara, labda sasa hivi kwa kuwa nawapa ninyi (waandishi wetu) hizi
taarifa ndiyo wanaweza na wao kujua kinachoendelea,” kilisema chanzo
hicho.
NDUGU WASAKWA Wakati gazeti hili
linakwenda mtamboni, lilifanya jitihada za kuwatafuta ndugu wa Jack
waishio jijini Dar lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda kwani namba
zao za simu zilikuwa hazipatikani. Hata hivyo, rafiki wa karibu wa
familia ya Jack ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini alisema
wamezipokea habari hizo kwa furaha kwani kulikuwa na hofu kubwa kuwa
huenda ndugu yao akanyongwa.
“Ndugu, jamaa na marafiki wa karibu na
Jack wameipokea hukumu hiyo kwa furaha maana walikuwa wakihofia adhabu
ya kunyongwa ambayo inatolewa zaidi nchini China,” alisema rafiki huyo
wa familia. JUX NAYE Ili kuzidi kujiridhisha zaidi, mapaparazi wetu
walimtafuta rafiki wa karibu wa Jack ambaye alikuwa akitajwa kuwa mpenzi
wake, Juma Khalid 'Jux Vuitton' lakini simu yake iliita bila
kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE Jack alikamatwa Desemba 19,
mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito
wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok
nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong
Kusini mwa China.
No comments:
Post a Comment