Msanii wa Hip Hop kutokea Mwanza, Godfrey Tumaini aka Dudu Baya amesema kuwa majanga anayopata kwenye mahusiano yake yanatokana na kutompata mwanamke anayemhitaji.
Akizungumza na Mkasi TV hivi karibuni, Dudu Baya amesema wanawake wengi anaokutana nao wanakuwa ni machizi.
“Kwanza
sijabahatika kukutana na mwanake ambae mimi namtaka, nafikiri
Mungu bado hajanipa huwaga nakutana na machizi, kwa sababu mimi
sipendi, mwanamke aliyelelewa na kufundwa vizuri vitu vya ndani huwezi
ukavitoa
nje.
Kwa mimi binafsi siongeagi kwa wanaume wengine, napenda sana siri za
familia zibaki kuwa siri za familia. Kwa mfano huyu jinsi alivyoenda
kwenye media asitarajie nimtamrudia kabisa, ile tabia ya kwenda kwa
jirani na kanga moja ikianguka? Kweli kabisa kicheni party zinaendelea
lakini hazisaidii kitu chochote,” alisema.

No comments:
Post a Comment