Thursday, 10 July 2014

Vera Sidika (mrembo wa Kenya) aanzisha app yake ya simu kwenye Google Store kwaajili ya picha za ‘asset’ yake


Vee3
Well, well, well, mrembo wa Kenya aitwaye Vera Sidika a.k.a Vee Baby aliwahi kukiri mwenyewe kuwa mwili wake ndio biashara yake katika Interview aliyofanyiwa na Larry Madowo nchini Kenya kwa mujibu wa Nairobiwire, na inavyoonekana hayuko nyuma na kanuni za biashara, si wote tunajua ‘biashara ni matangazo’? najua umesema ndio.

vee1
Mrembo huyo ameanzisha application yake ya simu inayoitwa jina lake ‘Vera Sidika’ inayopatikana ‘Google Play Store’, kwaajili ya kuwarahisishia mashabiki wake (wateja) kupata huduma ya picha za ‘asset’ yake kwa urahisi zaidi.LOL!
Vera App
Ndivyo inavyoonekana ukiisha download kwenye simu

Kama una smart phone jaribu kusearch ‘Vera Sidika’ kwenye Google Play, na utakapo install utakutana na picha mbalimbali za ‘asset’ ya mrembo huyo.
Application hiyo imewekwa kwenye kitengo cha burudani na ina maelezo mafupi tu yanayosomeka ‘A Kenyan Socialite’.
vee2
Huyu ndiye video vixen aliyesababisha video ya P-Unit ‘You Guy’ kufungiwa Kenya kutokana na kuwa ‘too sexy for TV’. Pia ameonekana kwenye video ya Prezzo ‘My Gal’.

Vee4

No comments:

Post a Comment