Tunguli za kichawi zikiwa juu ya kaburi la Marehemu Recho Haule.
AMA kweli duniani imani imekwisha!
Ikiwa inakaribia miezi miwili tangu kifo cha msanii wa filamu Bongo,
Rachel Leo Haule, vitu vya kutisha vinavyoashiria mambo ya uchawi
vimekutwa juu ya kaburi lake, Kinondoni jijini Dar.
Tukio hilo la kustaajabisha, lilidaiwa
kutokea Alhamisi iliyopita katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam.Kwa mujibu wa chanzo chetu, ndugu wa marehemu mmoja ambaye
hakujulikana jina walikuwa kwenye makaburi hayo wakifanya kumbukumbu
mbalimbali ndipo walipokuta ‘madongoloji’ hayo juu ya kaburi la Recho.
paparazi alikwenda mpaka eneo la tukio na kukuta vitu hivyo ambavyo ni tunguri moja iliyoviringishwa shanga, kitambaa cha kanga chakavu, manyoya ya kuku, yai moja (huenda likawa viza) na vitu vingine ambavyo havikujulikana ni nini.
WALINZI WATAFUTWA
Baada ya kujionea vitu hivyo, paparazi walikwenda kuwauliza walinzi wa makaburi hayo kama walikuwa na taarifa hizo.Mlinzi mmoja aliyeonekana kuwa ni fundi wa kuzungumza lakini bingwa wa uoga, hasa kwa kuona mauzauza ya kutisha kama hayo ndiye aliyepatikana. Akasema:

“Ah! Hivyo vitu vimetupwa na nani? Kuna watu walikuwa wakitembelea makaburi ya ndugu zao ina maana hawakuviona hivyo vitu?
“Lakini huyo mtu aliyewapigia simu mngemuuliza yeye, anaweza kuwa aliwaona walioviweka. Mimi siwezi kwenda sasa hivi kwenye hilo kaburi.”

NDUGU WA MAREHEMU WENGINE
Ingawa mlinzi huyo alishindwa kwenda kushuhudia tukio hilo, lakini watu waliokuwa wakisafisha makaburi ya ndugu zao walifika kwenye kaburi hilo kujionea madongoloji hayo.
Miongoni mwa waliofika na kuwa mashuhuda ni mama mmoja aliyedai ni mlokole wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kimara- Temboni jijini Dar ambaye alikataa kutaja jina lake.
Mlokole huyo alivikemea vitu hivyo kwa Jina la Yesu kisha akasema havina tena mamlaka ya kishetani kwa wakati huo na vimebaki kuwa takataka baada ya kuvipiga Neno la Mungu.

BABU ASEMA NI NDUMBA
Shuhuda mwingine alikuwa ni kijana mmoja aliyekwenda kujengea kaburi la mteja wake ambaye alishtushwa na mauzauza hayo na kusema hali inatisha! Baada ya kijana huyo, babu mmoja aliyekutwa eneo hilo alisema vitu hivyo ni ndumba maarufu sana mkoani Tanga ambapo alisema anaifahamu ndumba hiyo ambapo wachawi walikwenda kuwangia kaburi hilo na kujaribu kuivuta nyota ya marehemu.

Babu huyo aliongeza kuwa, wachawi hao
walichelewa kwani kwa kawaida kafara kama hiyo hufanywa siku saba baada
ya mwili wa marehemu kuzikwa.
“Mara nyingi nyota za wafu huweza kutumiwa na watu walioko duniani ingawa wakati mwingine mtumiaji wa nyota hiyo anaweza kupatwa na madhara makubwa ikiwemo kifo cha ghafla.
“Hawa ni cha mtoto tu, walikuja kulichezea hili kaburi lakini wamechemsha,” alisema mzee huyo.

SAGUDA WA RECHO SASA
Baada ya hapo, paparazi alimsaka aliyekuwa mchumba wa marehemu Recho, George Saguda ambaye alisema wao kama familia hawahusiki na tukio hilo na kudai hiyo itakuwa ni mipango ya washirikina.

Saguda akaenda mbele zaidi kwa kusema:
”Nitakwenda kukutana na walinzi wa makaburi wanieleze kinagaubaga
kulikoni kaburi la mchumba angu kuchezewa hivyo.”
No comments:
Post a Comment