Sunday, 27 July 2014

NSSF YAFUTURISHA WASTAAFU WAKE MKOA WA TANGA


Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (kulia), akishiriki katika futari iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga pamoja na wadau wake. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu na Kaimu Mkurugenzi wa NSSF, Chiku Matesa.

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limejipanga kuhakikisha linaboresha mfuko huo kwa kuwafikia wakulima na wafugaji nchini kote ili kupanua wigo kwa wanachama wake.

Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa, wakati akizungumza katika hafla ya kufuturisha wastaafu (PENSHENI) pamoja na wadau wa mfuko huo iliyofanyika katika hotel ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.

Alisema kuwa  wakulima na wafugaji wamekuwa wakisaulika hivyo kama shirika limeona vema kuwafikia ikiwemo kuwapatia elimu ambayo itawasaidia kujiunga na mfuko huo.

‘Sisi  kama shirika tumeona itakuwa ni vizuri zaidi kuwafikia wakulima na wafugaji ili kuweza kujiunga na mfuko wetu ambao unamafao uzazi, kuumia kazini, Kustaafu na mengineyo'.

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema shirika limeanzisha mpango wa kutoa mikopo kwa wanachama wake kupitia Saccos ambapo utalenga kuwawezesha wanachama wa mfuko  huo kujikwamua kiuchumi.

Naye  Mkuu wa Wilaya Tanga Halima Dendego aliwataka  wafanyakazi waliojiajiri na walioajiriwa ikiwemo wa mashambani kujiunga na mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF ili kuweza kujiwekea akiba hasa ya uzeeni.


“Nawaasa hawa wafanyakazi wajiunge na mfuko huu kwani unafaida kubwa hasa unapostaafu unakuwa na uhakika wa kuishi maisha bora yasiokuwa na wasiwasi’’alisema Dendego. 

Principle Operation Officer wa NSSF, Joyce Mruma akigawa zawadi kwa wastaafu wa NSSF wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na shirika hilo. 
Kaimu Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Tanga, Emmanuel Masika akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga.
Baadhi ya maofisa wa NSSF wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya wastaafu wa NSSF Mkoa wa Tanga wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kufuturisha wastaafu hao iliyoandaliwa na NSSF.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu akizungumza katika hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), iliyofanyika mkoani Tanga.
Meneja wa Mafao wa NSSF, James Oigo akijibu maswali ya baadhi ya wastaafu waliotaka ufafanuzi kuhusu huduma mbalimbali za shirika hilo. 
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Maryam Muhaji hafla ya kufuturisha wastaafu iliyofanyika Mkoa wa Tanga. 
Baadhi ya wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (katikati).
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (katikati), wa pili kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Alhaji Juma Luwuchu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa (wa  tatu kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji, Maryam Muhaji.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu, (kushoto)  akishiriki futari.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (wa tatu kushoto), akishiriki katika futari iliyoandaliwa na NSSF kwa ajili ya wastaafu wa Mkoa wa Tanga pamoja na wadau wake. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu na wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa NSSF, Chiku Matesa.
Wastaafu na wadau wa NSSF Mkoani Tanga wakijumuika katika futari.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Chiku Matesa akiwashukuru Wastaafu na Wadau waliohudhulia futari iliyoandaliwaa na mfuko huo.
Watoto wanaoishi katika Kituo cha Kulelea Watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Barabara ya 7 Mkoani Tanga wakiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa katika futari iliyoandaliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa ajili ya Wastaafu na Wadau wa Mfuko huo iliofanyika mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment