Staa wa kitambo kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Stanley MsunguTukio hilo lilijiri nje ya Mgahawa wa
Great Wall uliopo Masaki jijini Dar, usiku wa saa saba ambapo kulikuwa
na tafrija ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo
Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
“Dah! Kuna watu wana uhuru kweli na ndoa
zao, yaani Bonita amefunga ndoa juzijuzi tu, mumewe amelala nyumbani
yeye anahangaika huku na Msungu.
...akijificha kukwepa Kamera.“Kama huamini nenda kwenye gari
ukajionee wanachofanya Msungu na Bonita au hadi tufanye sisi ndiyo
mnatupiga picha?” alihoji mmoja wa waigizaji walioalikwa kwenye hafla
hiyo ambaye jina tunalihifadhi akimsisitiza mwanahabari wetu kwenda
kunasa tukio hilo.
Mke wa mtu anayedaiwa kuchepuka na Stanley Msungu.Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo,
paparazi kama kawaida yake lilinyata hadi lilipokuwa gari la Msungu
kisha kunasa tukio hilo ambapo Bonita alikuwa akijificha asionekane
vizuri huku Msungu akiwa katika hali ya kutaharuki.
“Kaka mke wa mtu huyu, utaniharibia mimi
na yeye kwa mumewe, achana na hayo mambo kaka njoo tuzungumze,” alisema
Msungu akijitetea huku Bonita akiomba kamera ya paparazi iishe chaji
ili zoezi la kupiga picha lisiendelee kabla ya kuondoka eneo hilo kwa
spidi na kutaka kumgonga paparazi.
No comments:
Post a Comment