Zikiwa ni
takribani wiki tatu tangu tasnia ya muziki wa injili nchini kumpoteza
mmoja wa waimbaji wake marehemu mchungaji Debora Saidi, taarifa ambazo
tumezipata ni kwamba mwimbaji mwingine wa muziki wa injili Orida Njole
amefariki dunia mchana wa leo katika hospitali ya Temeke jijini Dar es
salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.
Orida ambaye mpaka umauti unamfika mchana wa leo ilikuwa bado
haijajulikana nini hasa kinamsumbua lakini alikuwa ameishiwa damu sana,
mpaka umauti unamkuta alikuwa anatamba na album yake iitwayo 'Duniani tu
wapitaji' huku kwa mujibu wa watu waliomfahamu marehemu wameeleza
kwamba alikuwa mtu mchangamfu wakati wote wakati wa uhai wake na kwamba
wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo chake.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe!
![]() |
| Marehemu Orida akiwa na mtoto yatima katika kituo cha Tosamaganga Iringa alipotembelea kituoni hapo |



No comments:
Post a Comment