Akizungumza kwa kujiamini mbele ya
paparazi, juzi Jumatano pande wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, Kajala
alisema: “Wema ni mnafiki kabisa. Upatanisho wetu ni wa uongo. Mimi
moyoni nimeondoa kinyongo lakini mwenzangu naona kama bado ana donge
moyoni.”
Kajala alisema hayo alipoulizwa na
paparazi, sababu ya kutoonekana kwenye tukio la futari lililofanyika
nyumbani kwa mama mzazi wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura
Kassim ambaye ni mkwe wa shosti wake huyo.
Katika tukio hilo, mama Diamond
alifanyiwa sapraizi ya nguvu alipokabidhiwa gari kali aina ya Toyota
Lexus Harrier kama zawadi ya bethidei yake, ambayo ilitolewa na meneja
wa Diamond, Babu Tale kwa niaba ya mwanamuziki huyo ambaye alikuwa
safarini nchini Marekani.
“Tunakubaliana kuwa kitu kimoja lakini
mwenzangu anaonekana ana kinyongo. Hebu angalia, anawezaje kuacha
kunialika kwenye shughuli muhimu kama ile kama kweli tumepatana? Mbona
amealika watu wengi lakini mimi ameniacha? Wema aache unafiki bwana.
“Mbaya zaidi, hivi juzi tu ameweka picha
ya msichana mmoja anayekaa China, huyu mdada anaitwa Sabrina, niliwahi
kugomabana naye, lakini yeye amemuweka Instagram na kumwandikia maneno
kibao ya kumsifia akim-wish happy birthday, hapo si kama ananisimanga?
Wema si mkweli,” alisema Kajala.
Akizungumzia ishu hiyo, siku ya tukio
Wema alisema: “Ukiniuliza kuhusu Kajala kutokuwepo hapa, kwa kweli
utakuwa kama unanichanganya tu maana leo sijashika simu muda mrefu sana.
“Hata ujio wangu hapa nilikurupushwa, ndiyo maana sijakumbuka kumuita Kajala, lakini tuko vizuri na mara ya mwisho tumeongea jana (Jumapili) usiku tu,” alisema Wema.
“Hata ujio wangu hapa nilikurupushwa, ndiyo maana sijakumbuka kumuita Kajala, lakini tuko vizuri na mara ya mwisho tumeongea jana (Jumapili) usiku tu,” alisema Wema.
No comments:
Post a Comment