Tukio la ujambazi ambalo liliua watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi, limechukua sura mpya baada ya silaha waliyokuwa wakitumia majambazi hao kugundulika kuwa ilikuwa ikimilikiwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Sospeter Peter Manyika ambaye kwa sasa yuko rumande.
Kukamatwa
kwa Manyika kumethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha,
Liberatus Sabas lakini hakuwa tayari kusema chochote juu ya kuwekwa
rumande kwa askari huyo.
"Ni
kweli tulimkamata (Manyika) baada ya kufanya uchunguzi na kugundua kuwa
silaha waliyokutwa nayo majambazi ni mali yake," alisema bila ya
kufafanua chochote.
Vyanzo
vya habari kutoka ndani ya jeshi la polisi vilisema kuwa Manyika
alikamatwa Julai 9 mwaka huu akiwa kazini Ngorongoro, baada ya kubainika
kuwa silaha hiyo ilikuwa mali yake.
Habari
ziliendelea kusema kuwa Manyika ambaye ni dereva wa gari kubwa la FFU
anamiliki silaha aina ya shotgun namba A 947514 M – Pump Action
iliyotengenezwa Marekani.
Siku
ya tukio la kuuawa kwa majambazi hao watatu ambao walikuwa wakitumia
gari aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T 762 CWE, walikuwa
wanakwenda kupora fedha katika kampuni ya Arusha Ceramic Centre
inayojishughulisha na utengenezaji wa vigae.
Majambazi
hao waliuawa Julai 4 mwaka huu saa 10:20 jioni jirani na Kiwanda cha
Bia (TBL) eneo la Njiro Jijini Arusha na silaha hiyo ilikuwa na risasi
tatu.
Majambazi
hao walitambuliwa kwa majina ya Selemani Walii(25) mkazi wa Kaloleni
Jijini Arusha, Walter John (30) na mdogo wake Fred John (21) wote wakazi
wa Sekei wilayani Arumeru mkoani Arusha.

No comments:
Post a Comment