Marehemu Daniel Anael Lema enzi za uhai wake
Mwili
wa Daniel Anael Lema, aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada
ya sheria katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt. Augustino, Tawi la Iringa
(Ruaha University College – RUCO) umeagwa leo na kusafirishwa kuelekea mkoani kwao kilimanjaro kwa mazishi.
Wanafunzi
wa chuo hicho na wananchi wa manispaa ya Iringa walioguswa na tukio
hilo walijitokeza katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambako shughuli ya
kuuga mwili huo ilifanyika.
Jeshi
la Polisi mkoani iringa linawashikilia watu wanne ambao ni walinzi
wa duka usalama waliokuwa wakilinda nyumba moja ya kulala wageni iliyopo
Kihesa katika manispaa ya Iringa kwa tuhuma ya kumchoma moto
mwanafunzi huyo.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa Ramadhani Mungi
alisema tukio hilo lilitokea Juni 24 majira ya saa tisa usiku baada ya
wasamaria wema kutoa taarifa polisi kuwa kuna mtu anatembea akiwa
anawaka moto.
Mungi
alisema mara baada ya kupata taarifa hiyo Jeshi la Polisi lilifika
katika eneo hilo na kumkuta Daniel Lema (25) akiwa ameanguka chini
huku akiwa amefungwa mikono nyuma.
Kamanda
huyo aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mussa Nganga (28), Costa
Mgayuka (38), Steven Kalole (24) na Samson Peter (24) wote wakazi wa
Kihesa.
“Tulipopata
taarifa tulifika eneo hilo kwa haraka na tukamkuta ameanguka chini
tulimfungua ile mikono na kumchukuza vizuri tulimkuta akipumua kwa shida
ndipo tukamkimbiza hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa kwa ajili ya
kupata matibabu.”alisema Kamanda Mungi.
lisema
kuwa mwanafunzi huyo alikuwa baa moja inayoitwa Inbox bar
inayomilikiwa na Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Frederick Mwakalebela
akipata kinywaji huku akiangalia michuano ya mpira wa miguu (kombe la
dunia) ambayo inaendelea nchini Brazili.
“Mwanafunzi alikuwa anaangalia michuano hiyo ya mpira wa miguu kwenye baa hiyo na baada mpira
huo kuisha aliondoka na kuelekea nyumbani kwako Kihesa kabla ya kufika
nyumbani eneo hilo kuna nyumba ya kulala wageni iitwayo Glory lodge
ambapo pembeni yake kuna grocery moja iitwayo Glory grocery akaingia
hapo akifikiri ipo wazi ili aendeleze kinywaji,” alisema.Alisema
wakati akigonga mlinzi wa nyumba ya kulala wageni Glory lodge ambae ni
mmasai aitwaye Mussa Nganga alimuona na kumuita ndipo kijana akakimbia
na baada ya kukimbialimfukuza na kuwaita wenzake watatu na kumfanyia kitendo kama hicho.”alisema Mungi.
Baada
ya kufikishwa Hospitali ya Rufaa ya Iringa, Lema aliendelea na matibabu
yake mpaka alipokutwa na mauti jana majira ya saa nane mchana.
No comments:
Post a Comment