Watu watano wanadaiwa kuuawa katika
shambulizi lilifanywa na kundi la watu wenye bunduki katika eneo la
Pwani ya Kenya, karibu na eneo la Mpeketoni ambalo wiki yalifanyika
mashambulizi mawili yaliyosababisha vifo vya watu 60.
Kwa mujibu wa BBC, maafisa wameeleza
kuwa watu wenye silaha walivamia kijiji cha Witu, kilichoko kilometa 15
kutoka mji wa Mpeketoni, Jumanne alfajiri (Leo).
Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hili la tatu.
Kundi la Al-Shabab lilidai kuhusika na mashambulizi mawili ya wiki iliyopita katika eneo la Mpeketoni karibu na Lamu.
Hata hivyo, rais Uhuru Kenyatta alipinga na kudai kuwa mashambulizi hayo yanatokana na uchochezi wa wanasiasa wapinzani
No comments:
Post a Comment