Mmoja wa mastaa wa kibongo ambaye
ameonyesha kufuatilia michuano hii pamoja na wachezaji shiriki ni Jokate
Mwegelo, ambaye mtangazaji wa TV, muigizaji na mmiliki wa lebo mavazi
na fashion kiujumla ya Kidoti.
Tangu kuanza kwa michuano hiyo Jokate
amekuwa akiposti posti tofauti kuhusiana na michuano hiyo, huku
akionyesha namna anavyomkubali mwanasoka bora wa dunia Cristiano
Ronaldo, mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno
inayoshiriki kwenye kombe la dunia mwaka huu.
“Ronaldo ni mchezaji mzuri, anajituma
uwanjani na anafunga magoli akiisadia timu anazochezea. Ana nidhamu ya
kazi yake na akiifanya anaifanya kiuhakika na ndio maana tangu akiwa
Manchester United nikajikuta namshabikia. Pamoja na hayo kitu kingine
ambacho kinanifanya kumkubali Ronnie, ni namna ambavyo anajitoa kusaidia
watu wasiojiweza, kama tulivyosikia juzi ametoa kiasi cha zaidi ya
millioni 100 za kitanzania kusaidia matibabu ya mtoto aliyekuwa na
matatizo fuvu la ubongo kujaa damu.”
No comments:
Post a Comment