Wednesday, 25 June 2014

Tunaomba Radhi kwa Picha: Kikongwe auawa kinyama kwa kukatwa Shoka kichwani huko Kahama









Bibi
mmoja Mkazi wa mtaa wa Nyahanga, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga,
Rebeka Sengasenga (82), ameuawa kwa kukatwa na Shoka kichwani kwa kile
kinachohisiwa kuwa ni imani za Kishirikina.


Kwa
mujibu wa majirani, tukio hilo limetokea  jana asubuhi katika Mtaa wa
Nyahanga, wilayani humo, ambapo Marehemu Rebeka alienda nyumbani kwa
mtoto wake Bundala Sengasenga alikokuwa ameitwa na mke wa Bundala
kusaidia kuanika Dengu.

Imeelezwa
kuwa Merehemu Rebeka ambaye alikuwa akiishi kwa mwanae mkubwa Stanley
Sengasenga katika mtaa huo alifika kwa Bundala  baada ya kuitwa na
Magreth Richard ambaye ni mke wa Bundala kwa ajili ya shughuli hiyo.
       

Katika
maelezo yake Magreth amesema Mama mkwe wake Marehemu Rebeka alifikia
sebuleni, na kwamba wakati yeye yuko nje, alimwona mtu ambaye hakuweza
kumfahamu akitoka sebuleni hapo na kukimbia ndipo alipoangalia na
kumkuta Rebeka ameuawa.

Taarifa
za awali zimedai, kabla ya tukio hilo  Magreth ambaye kwa sasa
anashikiliwa na jeshi la polisi mjini Kahama kwa mahojiano alienda
nyumba ya jirani kuazima Shoka, ambalo baadaye limekutwa kwenye shimo la
maji taka nyumbani hapo.
Anayeshikiliwa akilia kwa uchungu ni Magreth anayehisiwa kuhusika na tukio hilo.

 
Shoka
hilo limepatikana baada ya mbinu za kiupelelezi za Jeshi la Polisi
kuagiza gari la maji taka kuyavuta maji hayo baada ya majirani kudai
hawajaona mtu aliyekimbia na shoka muda huo katika mwelekeo ambao
Magreth ameelekeza.

Jeshi
la Polisi wilaya ya Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti
katika hospitali ya Wilaya ya Kahama, huku upelelezi ukiendelea.
Mwili wa Marehemu Bi Rebeka ukiondolewa eneo la tukio kupelekwa Mochwari


No comments:

Post a Comment