Wednesday, 25 June 2014

SUAREZ AMNG’ATA MTU, ITALIA YATUPWA NJE





TIMU ya taifa ya Uruguay imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia nchini Brazil, lakini kituko ni straika wa timu hiyo, Luis Suarez kumng’ata beki wa Italia kwenye Dimba la Das Dunas.
Beki wa Italia, Giorgio Chiellini akionyesha sehemu aliong'atwa na Suarez.
Uruguay imefuzu hatua hiyo baada ya kuifunga Italia bao 1-0 katika mechi ya mwisho ya Kundi D ikiungana na Costa Rica ambayo ilitoka suluhu ya 0-0 dhidi ya England katika mechi ya mwisho pia kwenye Uwanja wa Mineirão.
Ikicheza pungufu baada ya Claudio Marchisio kupewa kadi nyekundu katika dakika ya 59 kwa kucheza vibaya, Italia ilijikuta ikitumia muda mwingi kucheza mpira wa kuzuia, huku Uruguay ilifanya mashambulizi mengi.
Bao pekee lilifungwa kwa kichwa katika dakika ya 81 na Diego Godin ambaye ndiye nahodha, kutokana na mpira wa kona.
Suarez alifanya kituko cha kumng’ata begani Giorgio Chiellin lakini mwamuzi hakuona tukio hilo, hivyo kutotoa adhabu yoyote.
Mara baada ya kung’atwa, Darmian alilalamika kwa mwamuzi huku akimuonyesha bega lake lakini hakuna uamuzi wowote uliochukuliwa.
Luis Suarez (kulia) wakiwa chini baada ya kumng’ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini  kwenye Dimba la Das Dunas.
Katika mechi ya England ambayo ilikuwa ikikamilisha ratiba, ilitumia wachezaji wengi ambao hawakuwemo kwenye mechi mbili za awali, ilishindwa kupata ushindi hiyo, kumaliza michuano ikiwa na pointi moja.
Kinara wa Kundi D ni Costa Rica kwa kuwa na pointi saba, wanaofuatia ni Uruguay pointi sita, Italia (3) na England (1).
Wachezaji wa timu ya Uruguay wakishangilia bao lao lilofungwa kwa kichwa katika dakika ya 81 na Diego Godin na kuwatoa Italia kwenye Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment