Mwizi ajisalimisha kwa Yesu na kuokoka dakika chache baada ya kuponyoka kipigo
Mtu mmoja ambaye alikuwa akishiriki
vitendo vya wizi alijikuta akimpa Yesu maisha yake hapo jana mara baada
ya kukimbilia kanisa la The Oasis Healing Ministries lililopo nyuma ya
jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es salaam, mara baada ya mwizi huyo
kukimbilia kanisani hapo akisalimisha maisha yake baada ya kuiba
alikotoka.
![]() |
| Mwizi akifanyiwa maombi akiwa ndani ya gari la polisi. |
Mwizi
huyo ambaye hata hivyo GK haikupata jina lake, mara baada ya kukimbilia
kanisani hapo, aliweza kuhubiriwa neno la Mungu ambalo alilipokea na
kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake na kuahidi kuendelea
kumshika na kumkiri Yesu, hata kokote atakapopelekwa na jeshi la polisi
ambao walifika kanisani hapo kumchukua mwizi huyo.
![]() |
| Maombi yakiendelea, alipata neema ya ajabu kwakweli. |
Tukio la mwizi huyo kumpokea Yesu
lilipokelewa kwa shangwe na waumini wa kanisa hilo ambao walishindwa
kuzuia furaha hiyo hata mwizi huyo alipopandishwa kwenye gari ya polisi,
ambapo mchungaji alimuombea huku mwizi huyo akionekana mwenye utulivu.
![]() |
| Maisha yake amempa BWANA. |



No comments:
Post a Comment