MSICHANA ALIYEPEWA MATESO MAKALI NA KUCHOMWA NA PASI ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI
Msichana
Yusta Lucas wa miaka ishirini aliyefungiwa ndani kwa miaka mitatu huku
akipewa adhabu ya kung'atwa na kuchomwa na pasi ameruhusiwa kutoka
hopitalini baada ya hali yake kuendelea vizuri huku jeshi la polisi
likikamilisha uchunguzi na mtuhumiwa kufikishwa mahakamani tarehe 11
Juni mwaka huu.
ITV
imefika katika hospitali ya Mwananyamala alikokuwa amelizwa Yusta Lucus
na kukutana na ndugu zake akiwemo mama ake mzazi ambaye amefafanua kwa
uchungu hali aliyomkuta nayo binti yake na hatua alizochukua mara baada
ya kupokea taarifa za tukio hilo.
Kaka
wa Yusta licha ya kutoa shukrani kwa msamaria aliyetoo habari za mdogo
wake kwa jeshi la polisi ameelezea kuendelea kusikitishwa na kitendo
hicho cha kinyama na kutoa wito kwa Watanzania kuwa na moyo wa kusaidia
wale wote wanaopatwa na matatizo kama hayo.
No comments:
Post a Comment