Mmiliki wa nyimbo za Bob Marley aamuliwa
Bob Marley
Mzozo wa kisheria juu ya nani anayemiliki baadhi ya nyimbo maarufu za reggae duniani umemalizika mjini London.
Nyimbo hizo zilizotungwa na kuimbwa na msanii Bob Marley zimekuwa ziking'ang'aniwa na kampuni 2 pinzani juu ya umiliki wao.
Jaji
katika mahakama kuu, Richard Meade alikata kesi ambapo kampuni ya Cayman
Music ilikuwa inadai kumiliki nyimbo 13, miongoni mwao wimbo uliopata
umaarufu 'No Woman, No Cry' kuwa haina haki nazo tena.
Kampuni
hiyo ilikuwa imedai kuwa nyimbo hizo hazikujumuishwa walipouza baadhi
ya haki zake kwa kampuni nyingine mnamo mwaka wa 1992.
Kampuni
ya Cayman imesema kuwa Bob Marley aliandika nyimbo hizo chini ya majina
tofauti, lakini Jaji ameamua kuwa bado kandarasi waliouzia inafunika
nyimbo zote hizo.
Bob Marley alifariki mwaka wa 1981 baada ya kuugua maradhi ya saratani kwa muda.Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment