MJANE mmoja
(jina linahifadhiwa kwa sababu za maadili) (24) mkazi wa Kijiji cha
Omuga, Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara amefanyiwa ukatili wa kutisha wa
kusimikwa kijiti sehemu zake za siri na shemeji zake ili kulazimishwa
kuhama baada ya mumewe kufariki dunia.
Msichana
anayedaiwa kufanyiwa ukatili wa kutisha wa kusimikwa mti sehemu zake za
siri na shemeji zake ili kulazimishwa kuhama baada ya mumewe kufariki
dunia akionyesha mti uliohusika kwenye tukio hilo
WANANCHI zaidi ya 500 wa Kijiji cha Moivaro na Chekereni katika Kata ya Moshono, wilayani Arumeru
Baba
mzazi wa mjane huyo, Alex Allal aliliambia gazeti hili kuwa mara
baada ya kupata taarifa za ukatili huo aliofanyiwa mwanaye aligundua
tayari alishatimuliwa kwake akawa anatangatanga na mtoto wake mdogo wa
kiume mwenye miaka saba.
Baba huyo alidai amefedheheshwa na kitendo cha shemeji wa binti yake kwa kumpiga kisha kumfanyia ukatili huo.
“Baada
ya kufanyiwa unyama huo, tuliripoti polisi na kupewa RB namba
UTE/RB/256/2014 na mmoja wa shemeji zake aitwaye Isaya Elphas alikamatwa
Mei 28, mwa huu na wengine kutoweka,” alisema.
Naye mjane huyo alidai kuwa, alianza
kunyanyaswa na shemeji zake hao baada ya mume wake Samwel Elphas kufariki dunia mwaka 2012.
Aliyataja manyanyaso aliyoyapata ni pamoja na kudaiwa kuporwa ardhi ekari mbili zilizokuwa na mashamba ya miwa, migomba,
mihogo na mahindi alizoachiwa na marehemu mumewe.
Alidai familia ya wakwe zake imemuomba aondoe shauri hilo katika vyombo vya dola ili wajadiliane na kupata suluhu.
No comments:
Post a Comment