Mauaji Mengine yawakuta Wakenya.....Watano wamevamiwa na kuuawa usiku wa kuamkia leo
Takriban watu watano wameuawa katika shambulizi jingine katika eneo la pwani ya Kenya usiku wa kuamkia leo.
Maafisa wanasema kuwa kundi la watu waliokuwa wamejihami walivamia kijiji cha Witu ambacho kiko umbali wa kilomita 15 kutoka mji wa Mpeketoni.
Hakuna aliyedai kufanya mashambulizi hayo hadi kufikia sasa.
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia,
al-Shabab lilikiri kufanya mashambulizi ya wiki jana katika mji wa
Mpeketoni karibu na Lamu.
Rais Uhuru Kenyatta, hata hivyo aliwalaumu wanasiasa kwa mauaji hayo.
Mkuu wa jimbo la Lamu, Stephen Ikua, alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo usiku wa kuamkia leo.
Al-Shabab, lilisema kuwa mashambulizi yao yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa kuwendelea kuwepo wanajeshi wa Kenya nchini Somalia.
Ndege za kivita za Kenya zilifanya mashambulizi
mengine dhidi ya kambi za wapiganaji wa Al Shabaab na kuwaua wapiganaji
80 mapema wiki hii.

No comments:
Post a Comment