majanga:mume amtwanga mkewe na mchi kichwani, alazwa hoi muhimbili kisa chaelezwa ni hawara !
Bi. Pamela Said akiwa katika maumivu makubwa.
Tukio
hilo la kusikitisha lilijiri Mei 23, mwaka huu nyumbani kwa wanandoa
hao, Mwembe-Supu, Ulongoni maeneo ya Gongo la Mboto, Dar muda mfupi
baada ya kutoka kwenye bata ndefu usiku.
Habari zilidai kwamba kabla ya kugeukia masumbwi, wanandoa hao walikuwa kwenye ‘pub’ yao iitwayo Milano iliyopo maeneo hayo wakijiachia kwa raha zao.
Habari zilidai kwamba kabla ya kugeukia masumbwi, wanandoa hao walikuwa kwenye ‘pub’ yao iitwayo Milano iliyopo maeneo hayo wakijiachia kwa raha zao.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, ilibainika kuwa siku hiyo majira ya saa 5:00
usiku, Alex, akiwa amepitiwa na usingizi simu yake iliita huku jina la
Salima likionekana kwenye ‘skriini’.
Ilisemekana kwamba Salima aliwahi kuwa mfanyakazi katika pub yao ambapo Pamela alimtuhumu kuwa na uhusiano na mumewe.
Ilisemekana kwamba Salima aliwahi kuwa mfanyakazi katika pub yao ambapo Pamela alimtuhumu kuwa na uhusiano na mumewe.
Ilidaiwa
kuwa Pamela alimuomba mumewe wakamtimua kazi Salima lakini amekuwa
akiendeleza uhusiano huku akipiga simu mara kwa mara hasa usiku kitendo
ambacho kilimchukiza Pamela.
Ilidaiwa kuwa baada ya kuona simu hiyo, Pamela alimuamsha mumewe ambaye alipokea simu hiyo na kuanza kujikanyaga na kukata simu ndipo alipompigia kwa namba yake na kuanza kujibizana huku akipokea maneno ya karaha bila kutegemea mazungumzo hayo yalimtia hasira Pamela ambaye alimuuliza kwa hasira mumewe huku akitaka kujua kuna nini kati yake na huyo Salima.

Ilielezwa
kuwa kitendo hicho cha mke kutaka kujua ukweli ndipo mumewe akaanza
kutoa maneno akidai kwamba atamuonesha kazi ambapo alichukua mchi wa
kinu na kuanza kumpiga nao maeneo ya usoni na mikononi hadi Pamela
akapoteza fahamu.
Ilisemekana
kuwa kelele za kipigo hicho kiliwashtua majirani ambao walisogea kwenye
nyumba hiyo ili kujua nini kinaendelea na kumkuta Pamela akiwa amezimia
jambo lililowafanya kutafuta msaada wa kumpeleka hospitali ili kuokoa
maisha yake.
Ilidaiwa
kwamba katika hali isiyo ya kawaida, mume wa Pamela alikataa na
kuwaambia wampeleke hospitali wenyewe, kwa kuwa kulikuwa na gari ikabidi
wamtafute dereva usiku huo na kumwahisha kwenye ‘dispensari’ ya karibu
iitwayo Kwa-Jose.
Baada
ya kumfikisha dispensari walikataliwa kutokana na hali ya Pamela kuwa
mbaya hivyo wakamkimbiza kwenye zahanati inayoitwa Jeshi, napo
walishauri mgonjwa huyo apelekwe Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Pamela
alifikishwa Muhimbili alfajiri ya saa 12:00 akiwa anatapika damu katika
hodi ya Mwaisela na kuanza matibabu kisha kutoa taarifa katika Kituo
cha Sitaki-Shari na kufunguliwa jalada la kesi namba STK/RB/70220/2014-
SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI.
Habari
kutoka kwa mmoja wa ndugu wa Pamela zilieleza kuwa kulitokea mvutano
mkubwa wa pande mbili ambapo Alex alitaka mke arudishwe nyumbani na
kuendelea na matibabu jambo ambalo lilipingwa vikali na kaka wa Pamela
akisema dada yake bado ana hali mbaya.
Akizungumza kwa tabu hospitalini hapo, Pamela alikiri kufanyiwa ukatili huo na mumewe.
No comments:
Post a Comment