KIFO CHA TYSON, KUNA KITU!, WACHUNGAJI NA MASHEHE WAMCHUKIA MTABIRI, WADAI NDIYE MCHAWI
Tatizo!
Huku macho ya waigizaji na wadau wake hayajakauka machozi kufuatia vifo
vya ghafla vya mwongoza sinema, Adam Philip Kuambiana (38) na mwigizaji
Sheila Leo Haule ‘Recho’ (26), tasnia imempoteza mwingine, mwigizaji,
prodyuza na mwongozaji filamu mahiri, George Otieno ‘Tyson’ (41).
Kufuatia
kifo hicho ambacho pia ni cha ghafla, wadau mbalimbali wa filamu,
wakiwemo wasanii wenyewe wamesimamia mawazo yao kwamba lazima kuna kitu!
Tyson
alifariki dunia Ijumaa usiku akiwa njiani kukumbizwa Hospitali ya Mkoa
ya Rufaa Mkoa wa Morogoro kufuatia ajali mbaya ya gari iliyotokea maeneo
ya Gairo, Morogoro.
Katika
ajali hiyo, mbali na marehemu walikuwemo watu wengine watatu ambao ni
dereva, MC Gladness Chiduo ‘Zipompa’ na mwingine aliyejulikana kwa jina
moja la Nick ambao walijeruhiwa vibaya na kupatiwa matibabu ya haraka.
WALIKUWA WAKITOKEA WAPI?
Gari walilopata nalo ajali ni Toyota Noah ambalo liliharibika mno. Wote walikuwa wakitokea Dodoma ambako Ijumaa mchana walirekodi kipindi na pia kutoa misaada ya madawati 60 kwenye Shule ya Msingi ya Chalula iliyopo Chamwino kupitia Kipindi cha Mboni Show kinachoongozwa na Mboni Masimba kupitia Runinga ya EATV.

Mboni yeye kama bosi wa msafara huo alikuwa kwenye gari jingine na watu kadhaa.
KISA CHA AJALI
Kwa mujibu wa chanzo, ajali hiyo ilitokea baada ya tairi la nyuma la kulia kupasuka ghafla kisha kufuatiwa na la mbele kushoto hali iliyosababisha gari hilo kupinduka na kubiringita mara tatu.

“Kwanza
ilipobiringita mara moja, Tyson alichomoka kwenye gari, likabiringita
tena mara mbili. Marehemu alipasuka sehemu ya kati ya paji la uso,”
kilisema chanzo na kuanza kulia.
MANENO YA MWISHO YA MAREHEMU
Chanzo kilizidi kusema kuwa wakati marehemu anazingirwa na roho wa mauti alikuwa akisema ‘najua nakufa lakini nasikitika kuwaacha wanangu.’

KUNA KITU
Kwa upande wa wasanii kutoka tasnia ya filamu Bongo waliozungumza na paparazi juzi, walikazia dhana ya kuwepo kwa kitu kinachoondoa uhai wa wasanii kwa njia ya kufumba na kufumbua.

“Haiwezekani
kila kukicha sisi tu. Tena ghafla. Aisee lazima kuna kiti japokuwa
hatujakijua ni kitu gani,” alisema msanii na kiongozi wa Kundi la Jakaya
Theatre, David Mponji ‘Lazi’.
Akaongeza:
“Lakini nataka kukwambia kwamba huu ni mpango wa Mungu kabisa ili
tufanye ibada. Unajua asilimia themanini ya wasanii hawaendagi kanisani
wala misikitini? Hapa sasa tunakumbushwa.”
JACOB STEVEN ‘JB’:
“Hii ni too much! Kweli kifo sasa hata mimi nakiona kiko karibu. Nadhani kuna kitu.”

WILLIAM MTITU:
“Da! Sijui mimi niseme nini. Nadhani iko sababu ya kujiangalia, inakuwa kama kuna kitu vile.”

JACQUELINE WOLPER:
“Siamini aisee! Yaani juzi tu Kuambiana, akaja Recho, leo Tyson! Mh! Pana kitu hapa. Afadhali tungekuwa tumelia mpaka tumekauka machozi.”

WACHUNGAJI, SHEHE WAMSHUKIA MTABIRI
“Ukisema tabiri maana yake umba jambo. Ndiyo maana hata kwenye maandiko Mungu alimwambia nabii mmoja atabiri mafuvu kuwa binadamu, ikawa hivyo.

“Sasa
huyu mtabiri (hakumtaja jina) ambaye amekuwa akisema wasanii watakufa
kwa wingi ndiye ‘mchawi’ wao maana anaumba vifo kwa wasanii,” alisema
Mchungaji Daniel Rashid wa Kanisa la EAGT Tegeta jijini Dar.
Naye
shehe aliyejitambulisha kwa jina la Hussein alipozungumza na paparazi
juzi alisema yeye anaamini mtabiri ambaye amekuwa akisema wasanii
watakufa ndiye mchawi wao.
“Kwanza kwa nini uwatabirie wenzako tu? Kuna nini hapo? Mbona sijawahi kusikia amejitabiria mwenyewe?” alihoji Shehe Hussein ambaye hakupenda kuuanika msikiti anaofanyia utumishi wake.

WOSIA MZITO KWA MASTAA
Katika hatua hiyo, viongozi hao wa dini walitoa wosia kwa mastaa wakisema kwamba katika hali kama hii hakuna njia mbadala zaidi ya kufanya ibada.
Walisema huenda pia vifo hivyo ni mpango wa Mungu ili kuwakumbusha kufanya ibada kwani wasanii wanaonekana muda mwingi wapo kazini kuliko kwenye nyumba za Mungu au hata kumkumbuka kwa maombi tu.

BONGO MUVI: HAKUNA KUREKODI FILAMU
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movies waliozungumza na paparazi juzi walisema wanasikitishwa na vifo hivyo kwani kwa sasa imefikia hatua kwamba wanakosa muda wa kurekodi filamu, muda mwingi wapo kwenye misiba.

“Hatumkufuru
Mungu kwani yeye ndiye muumba ila kusema kweli muda mwingi tunautumia
kuzika tu. Filamu za kurekodi zote zimesimama, maana da!” alisema msanii
mmoja akiomba hifadhi ya jina.
MWILI WA TYSON
Mwili wa Tyson ulitarajiwa kufikishwa Dar Jumamosi iliyopita kutoka Morogoro. Mjadala uliendelea hadi jioni ya juzi kwamba mwili wa marehemu ukazikiwe wapi kwa vile marehemu ni mwenyeji wa Kenya.

WAZAZI WAKE WAFICHWA
Habari za baadaye zilidai kwamba, hadi juzi jioni taarifa za kifo cha Tyson zilikuwa zimefichwa kwa wazazi wake kutokana na kile kilichodaiwa kwamba, hali zao kiafya ni ‘tiamajitiamaji’.

ASILI YA TYSON
Tyson alitua nchini mwanzoni mwa mwaka 2,000 akitokea Kenya. Alipofika alifanya kazi katika Kituo cha Runinga cha ITV akiwa ni prodyuza wa Kipindi cha Mambo Hayo.

Hapo
ndipo alipomwibua Yvone-Chery Ngatwika ‘Monalisa’ na kumwingiza kwenye
sanaa na baadaye kuwa mchumba wake ambapo mwaka 2001 walifunga ndoa ya
kanisani.
Baadaye
marehemu alijitoa ITV na kufanya kazi binafsi huku akiwa mwongoza
sinema mahiri Bongo. Amekuwa mwongozaji wa vipindi mbalimbali kama Mboni
Show cha Mboni Masimba, Wanawake Live cha Joyce Kiria na vipindi kibao
vya TV1.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina
No comments:
Post a Comment