Wednesday, 4 June 2014

HATIMAYE!! CHRIS BROWN ATOKA JELA, ANENA MAZITO

HATIMAYE!! CHRIS BROWN ATOKA JELA, ANENA MAZITO

Chris Brown atoka Jela
Chris Brown akiwa mwenye uso wa furaha baada ya kuachiwa huru
Hatimaye hitmaker  wa Loyal ‘Chris Brown’  ameachiwa huru asubuhi ya leo tangu awekwe kuzuizini katikati ya mwezi machi baada ya kukiuka kanuni za Rehab,  ingawa kuachiwa huko kunatajwa kuwa ni kwa muda mfupi kutokana na kukabilia na kibarua kingine cha kujibu mashtaka ya kesi yake ya pili ya kumshambulia shabiki mjini Washington DC na endapo atapatikana na hatia huenda akakumbwa na kifungo cha miezi 6  gerezani.
Akionyesha kila dalili za furaha, mwimbaji huyo hakuwa na budi zaidi ya kumshukuru mwenyezi mungu kwa kumuwezesha kutoka  nyuma ya nondo za jela ya LA County na kisha kumalizia kwa kuwasabahi mashabiki wake aliokuwa amewamisi kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
”Humbled and Blessed”,  ”Back to the music and the Fans”  na  ”Thank You God” hizo zilikuwa baadhi ya tweets alizoandika Brown kwenye ukurasa wake wa twitter.
Wafuasi wwa BrownMashabiki wa Chris Brown wakiwa wameshika mabango nje ya mahakama wakishinikizwa kuachiwa huru kwa jembe lao
Chris Brown Twitter

No comments:

Post a Comment