Wednesday, 4 June 2014

FILAMU MPYA YA SALMA JABU NISHA YAFICHUA SIRI NZITO

FILAMU MPYA YA SALMA JABU NISHA YAFICHUA SIRI NZITO

Salma Jabu Nisha /Tanzanian Actress
Nisha akiongea na mwandishi wa masainyotambofu.com leo majira saa saba alasiri, Nisha katika moja ya vitu alivyovizungumzia ni pamoja na maudhui ya Filamu yake mpya iitwayo ZENA NA BETINA,

Mwanadada huyo kutoka Bongo Movie's alisema kuwa ZENA NA BETINA imezungumzia dada zetu wanaofanya biashara ya ngono ndani na nje ya nchi hasa huko nchini china, Pamoja na wanawake wanaowachukuwa watoto wa kike kijijini kuwaleta mjini kisingizio kikiwa ni kuwapa ajira ya kazi za ndani alafu matokeo yake wanawauza kwa mijibaba yani kuwafanyisha biashara ya ngono.

Aliendelea kusema kwamba Filamu hio imeanika mambo hayo kwa lengo la kuwajanjarusha wanaodanganywa na kuifunza jamii kwa ujumla ili kuweza kulitokomeza tatizo hilo maana ni fedheha kwa watanzania. Alisema Nisha
Huu ndio muonekano wa kava rasmi la Filamu hio.

No comments:

Post a Comment