DRC yailaumu Rwanda kuwalinda M23
DRC yailaumu Rwanda kuwalinda M23
Serikali
ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imeikashifu serikali ya Rwanda kwa
kuwalinda wapiganaji wanaotuhumiwa kwa kusababisha mauaji ya halaiki
chini ya nembo ya wapiganaji wa M23.
Afisa
mmoja wa Serikali ya DRC ameiambia BBC kuwa imekuwa vigumu kwa serikali
yake kuwahoji zaidi ya wapiganaji 500 ambao wamekita kambi nchini Rwanda
licha yao kutuma ombi la kufanya hivyo yapata miezi saba iliyopita .
Zaidi
ya watu 800,000 walitoroka makwao haswa mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemkrasia ya Congo wakati wa mapigano hayo ya wenyewe kwa wenyewe.
Rwanda imekuwa ikipinga madai hayo na kusema kuwa imeshirikiana na serikali ya DRC.
Kundi
hilo la M23 lichukua silaha mashariki mwa DRC kuanzia Aprili 2012,
liliaumu serikali ya Kinshasa kwa kuwabagua jamii ya watutsi na pia
kupuuza makubaliano ya awali ya kusitisha mapigano.
Kundi
hilo hata hivyo lilishindwa katika mapigano yaliyoongozwa na jeshi la
Umoja wa mataifa likisaidiwa na majeshi ya serikali ya Congo mnamo
November 2013.
Wapiganaji hao walitorokea Rwanda na Uganda.
DRC yailaumu Rwanda kuwalinda M23
Katika mji wa Ngoma, mashariki mwa Rwanda mwandishi wetu alikumbana na wapiganaji hao ana kwa ana katika kambi nje ya mji.
Wengi
wao wanasema kuwa wamechoshwa na ngoja ngoja hiyo ambayo imedumu kwa
kipindi kirefu sasa na wanasema kuwa wangependa kuomba hifadhi nchini
Rwanda, kwani wanahofia kurejea ndani ya Congo.
Serikali ya Congo imetangaza kuwa itawapa msamaha wapiganaji hao.
Tulipoingia ndani ya kambi hiyo ,hali na taswira ilikuwa tulivu na shwari .
Kulikuwa na hema kubwa nyeupe, majengo kadha mbali na bustani iliyolindwa na nadhifu.
Wapiganaji hao wanalala sita katika chumba kimoja .
Wanajipikia wenyewe hadharani na hawaruhusiwi kuondoka kambini ila wanapokwenda kupata matibabu.
Japo taswira hiyo ni ya utulivu wapiganaji zaidi ya 100 wametoroka tangu kuzinduliwa miezi 15 iliyopita .
Wapiganaji wa M23 waomba hifadhi Rwanda
Kiongozi wao Jean Marie Runiga hana mipango yeyote ya kutaka kurejea nyumbani.
Runiga ambaye anatuhumiwa kwa mauji ya jinai na DRC ameomba hifadhi nchini Rwanda .
Mwenyewe haishi kambini,anakaa katika jumba alilokodishiwa na serikali karibu na kambi hiyo.
Afisa
wa Serikali ya DR Congo Francois Muamba,amesema kuwa Rwanda kinyume na
Uganda ,imekuwa ikijivuta sana katika swala kuu la kuwataka wale
wanaotuhumiwa kwa mauaji ya halaiki na makosa mengine dhidi ya binadamu
kufikishwa mahakamani .
Muamba
ameilaumu serikali ya Kigali kwa kuwalinda makamanda wanne wa M23
wanaoshtumiwa kwa kuongoza mauaji ya halaiki nchini DR Congo.
Anasema
Rwanda imezuia mahojiano ya wapiganaji hao licha ya kutakiwa
kuwawakilisha kwa vyombo vya usalama vya DRC.Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment