BABY MADAHA AFUNGUKA, "SIAMINI KAMA ADAM KUAMBIANA NA RECHO WAMEKUFA MPAKA NIONE MAKABURI"
MSANII wa
filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha (pichani juu) ambaye kwa
sasa yuko Kenya amesema kuwa, haamini kama kweli wasanii wa filamu Recho
Haule na Adam Kuambiana wamefariki dunia mpaka siku atakapoyaona
makaburi yao.
Maziko ya Msanii Recho yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
Akizungumza
na Ijumaa kwa njia ya simu, Madaha alisema ameshitushwa na vifo hivyo
na vimemfanya akose amani kutokana na namna walivyoondoka duniani
ghafla.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Adam Kuambiana.
“Nilitamani sana kuwepo lakini niko mpakani mwa Kenya na Uganda kuna ziara maalum ya kikazi naifanya.
Yaani bado siamini kama kweli wamefariki, mpaka nije nione walipozikwa,” alisema Baby Madaha.



No comments:
Post a Comment