Tuesday, 27 May 2014

‘SAUDA MWILIMA ACHA MKOROGO’



‘SAUDA MWILIMA ACHA MKOROGO’

Kama
kawa wiki iliyopita tulimleta kwenu prizenta wa Star TV, Sauda Mwilima
ambapo mlimuuliza maswali anayoyajibu wiki hii. UNGANA NAYE… VIPI









Prizenta wa Star TV, Sauda Mwilima.
KUHUSU BANGI?

Nasikia wakati unasoma ulikuwa unavuta bangi, je, ni kweli au? Andrew Kazala, Dar, 0717179570

SAUDA: Sijawahi kuvuta bangi na sijui inafanana vipi.
PONGEZI

Mara
utasikia oooh, Maimartha Jesse anauza dawa za kuongeza makalio au Lulu
Semagongo ana danguro la kuwauza mashoga lakini kwa Sauda Mwilima
sijawahi kusikia skendo yoyote ile, hakika wewe ni kioo cha jamii
hongera sana. Rocky Moshi, 0715289337


SAUDA: Nashukuru sana kwa hilo endelea kuniombea.
HUYU ANATAKA KUJUA

Sauda
kwanza hongera kwa kuwa wewe siyo mtu wa matukio, nataka kujua eti ni
kweli huwa unadaka mlungula kwenye kipindi chako cha Bongo Beat kwa
wasanii? John Ipembe, Shinyanga, 0713554815


SAUDA: Hapana, kipindi changu ni kwa ajili ya kuwasaidia wasanii.
NINI AMBACHO HATAKISAHAU?

Jambo gani ambalo huwezi kulisahau katika maisha yako? Anijay Nswillah, Mbeya, 0768538920

SAUDA: Siwezi kusahau nilipompoteza mtoto wangu.
HUYU ANAMSHAURI

Nakushauri uache mkorogo utapendeza zaidi hukuwa hivyo zamani. Bland, Mwanza, 0782527646

SAUDA: Asante lakini situmii mkorogo.
Sauda Mwilima akiwa na Zamaradi Mketemwa.
ANA WATOTO WANGAPI?

Sauda nakukubali sana unavyotangaza naomba kujua umezaa na una watoto wangapi? Abuu Sungura, Dar, 0654799098

SAUDA: Sina mtoto.
ETI ALIWAHI KUWA RADIO FREE?

Dada
Sauda mimi nakupenda sana kiukweli uko vizuri na unajitambua. Swali
langu, je, uliwahi kuwa mtangazaji wa Radio Free? Raphael, Morogoro,
0713850820


SAUDA: Asante kwa kunipenda, ni kweli mpaka sasa ni mtangazaji wa Radio Free na Kiss FM.
JE, ANA NDOTO ZA KWENDA BBC?

Sauda ulishawahi kufikiria kufanya kazi BBC au ndoto yako imetimia kufanya kazi Star TV? Bforshizzle, 0713775834

SAUDA: Kila mtu ana ndoto za kuwa juu hivyo na mimi siku ikitokea hiyo nafasi nitamshukuru Mungu na nitaenda.
HUYU ANATAKA KUFAHAMU

Dada
Sauda nakupongeza sana kwa kutokuwa na skendo, hongera, mimi ningependa
kujua wewe ni mtu wa mkoa gani na je, umeolewa? Saidi, Dar, 0715155580


SAUDA: Nashukuru, mimi ni Mmanyema wa Kigoma, nimeolewa.
MALENGO YAKE

Hongera kwa kazi na changamoto zake, vipi matarajio yako ya baadaye? Frances Mwakibete, 0717274027

SAUDA: Malengo yangu ni kufanya kazi nzuri ili nifike mbali zaidi pamoja na kuelimisha jamii zaidi.
VIPI KUHUSU KANUMBA?

Eti
inasemekana kuwa ulikuwa unatoka kimapenzi na mwigizaji nyota marehemu
Steven Kanumba, je, kuna ukweli wowote na una umri gani mpaka leo kwenye
fani ya utangazaji na unakumbana na vishawishi gani? Joel Kwanga, Dar,
0654066633
SAUDA:
Sijawahi na Kanumba hakuwahi kunitamkia mambo ya mapenzi, nina miaka
kumi kwenye utangazaji, vishawishi ni vya kawaida kwa kila mwanamke
kikubwa ni kujitambua tu.
YEYE NA SAIDA VIPI?

Wewe na Saida Mwilima ni ndugu? Sasa hivi yupo wapi? Neema Wangwe, Dar.

SAUDA: Saida ni ndugu yangu tumezaliwa tumbo moja kwa sasa amehamia London (Uingereza).
CHANGAMOTO ANAZOKUMBANA NAZO

Naikubali sana kazi yako ila kuna changamoto gani unazipata katika kazi yako ya utangazaji? Baraka Suleiman, Dar, 0784613349

SAUDA: Changamoto ni za kawaida tu siyo nyingi.
ANA KAZI GANI NYINGINE?

Hongera kwa kazi, je, tofauti na kazi ya uandishi na utangazaji unajishughulisha na nini? Jose, 0757904855

SAUDA: Ninafanya biashara, pia ni mshehereshaji kwenye shughuli mbalimbali na mambo mengine mengi.
ANATAKA KUJUA

Tangu uanze mapenzi yenu na mume wako mlishawahi kugombana? Reshima, Dar, 0716258570

SAUDA:
Hapana, hatujawahi kugombana, ikitokea ni vya kawaida tu vya kupishana
kauli, tunaongea yanaisha, haijawahi kutokea ugomvi mkubwa.
HUYU ANAHOJI

Namjua
dada Sauda alikuwa anaishi Morogoro maeneo ya Kigurunyembe karibu na
Rombo Bar, baba yake alikuwa anafanya kazi kiwanda cha seramiki, ni mtu
wa Mkoa wa Kigoma. Msomaji, 0712599020


SAUDA: Huyo ni dada yangu Saida, umetuchanganya.
ETI ALIWAHI KUSOMA DSJ AU TSJ?

Je, ni kweli Sauda uliwahi kusoma kati ya vyuo hivi DSJ au TSJ vilivyopo Ilala, Sharif Shamba, Dar? Muddy Madiley, 0652672805
SAUDA: Hapana sijawahi kusoma huko.

NANI ALIMVUTIA KWENYE UTANGAZAJI?

Mimi nataka kujua ulianza lini utangazaji na nani alikuvutia kwenye fani hiyo? Rashidi Gombe, Dar, 0712231852
SAUDA: Nilivutiwa
na dada yangu Saida, kipindi hicho nilikuwa shuleni yeye alikuwa
Mtangazaji wa TBC  kwa hiyo na mimi nilipomaliza shule nikafuata nyayo
zake.

No comments:

Post a Comment