Tuesday, 27 May 2014

SAMAHANI KWA PICHA: MAJAMBAZI DAR WAUA POLISI KINYAMA



SAMAHANI KWA PICHA: MAJAMBAZI DAR WAUA POLISI KINYAMA

Mwili wa jambazi mwingine ukiwa umeharibika vibaya baada ya kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira.









 Mwili wa askari aliyeuawa ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Temeke

Askari polisi mmoja wa kituo cha
polisi Chang'ombe, Mkoa wa kipolisi wa Temeke, ameuawa kikatili siku ya
ijumaa mchana baada ya kupigwa risasi ya kifua na majambazi waliokuwa
wanajaribu kutoroka baada ya kufanya tukio la kihalifu. Askari hao
waliokuwa doria katika eneo la Wailes walijikuta wakishambuliwa kwa
risasi na majambazi hao mara baada ya majambazi hao kujaribu kukimbia
katika eneo la tukio kwa kutumia usafiri wa pikipiki kipindi ambapo
askari polisi walikuwa karibu na eneo la tukio. Hata hivyo wakati askari
hao wakijaribu kuwafukuza majambazi hao wawili kwa lengo la kuwakamata
ndipo jambazi mmoja alitoa bastola na kumpiga risasi ya kifua askari
huyo na kufariki pale pale.




Mwili wa askari huyo ukiwa umehifadhiwa.



Hata hivyo katika harakati za kujaribu
kukimbia majambazi hao walianguka na pikipiki waliyokuwa wakitumia
ndipo wakaamua kutimua mbio mitaani na kuingia katika nyumba moja ambapo
walijificha na kujifanya kama ni wakazi wa eneo hilo, baada ya wananchi
na polisi kufika katika nyumba hiyo, baadhi ya majirani waliwaambia
polisi kwamba wameona watu hao wameingia katika nyumba hiyo. Baada ya
polisi kuingia waliwakuta watu hao wakiwa wametulia kama kwamba wao ni
wakaazi wa nyumba hiyo na wala hawajui lililotokea.




Mwili wa mmoja wa majambazi ukiwa chumba cha kuhifadhia maiti 


Baada ya kuwatambua watu hao, polisi
waliwatia nguvuni huku wananchi wenye ghadhabu waking'ang'ania kuwa
wanataka kuwaua sababu wameshaua askari mmoja. Baada ya vuta nikuvute
kati ya wananchi na askari hao ambao walikuwa wachache, wananchi
walifanikiwa kuwachukua majambazi hao kwa nguvu kutoka mikononi mwa
polisi na kuanza kuwapiga kwa silaha mbalimbali za kienyeji yakiwemo
mawe na marungu mpaka watuhumiwa hao wakapoteza maisha.




Mwili wa jambazi mwingine ukiwa umeharibika vibaya baada ya kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira.






Mwili wa askari polisi ukiwa umepakiwa kwenye gari ya polisi tayari kupelekwa hospitali ya Temeke kuhifadhiwa.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo
waliiambia blogu hii kwamba majambazi hayo kabla ya kupambana na polisi
walikuwa wamefanya uvamizi na kumuibia mwanamke mmoja mkazi wa eneo
hilo. Hata hivyo mali au fedha iliyoibiwa haikuweza kujulikana mara
moja.

No comments:

Post a Comment