Pinda Atetea mbio za Mwenge Asema zina Faida !...Kweli Jamani?
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ametetea umuhimu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru,
akisema ni jambo kubwa lenye manufaa ambalo moja ya faida zake ni
kuhimiza umuhimu wa kujitolea miongoni mwa wananchi katika kujiletea
maendeleo yao.
Aidha, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia
amesema mbio za Mwenge zinaeneza ujumbe wenye manufaa kwa jamii, kuliko
mikutano inayofanywa na kundi linalojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa).
Waziri Mkuu Pinda alishan- gazwa na mjadala ulioibuliwa na wabunge wa
upinzani bungeni jana kuona Mwenge kama suala lisilo na maana kwa taifa.
“Nimesimama kwa sababu nimesikiliza mjadala hapa, naona jambo hili
kubwa, linaonekana kama halina maana kwa taifa,” alisema Pinda na
kuongeza:“Kila mwaka, mbio za Mwenge huwa na kaulimbiu mahsusi kwa
sababu Mwenge huu huwa na fursa ya ku- fika maeneo mengi hivyo kufikisha
ujumbe kuhusu masuala mazito ya nchi kama elimu. Kwa hiyo, si sahihi
kabisa kuona Mwenge hauna maana.”
Alisema anafahamu kuwa wap- inzani wanaweza wasipendezwe sana na Mwenge kuhimiza suala la kujitolea miongoni mwa wananchi.
“Hili linaweza lisiwapendeze sana wenzetu wa upande wa pili. Mwenge
unahimiza suala la kujitolea katika shughuli zao za maendeleo.
“Wananchi wanahimizwa kuenzi moyo huo na wamekuwa wakifanya hivyo katika
shughuli mbalimbali za kijamii. Hili halina ukakasi hata kidogo.
“Hoja hapa imekuwa ni michango, lakini hivi Mwenge unakuja pale kwangu
Kibaoni, kwa ugeni huo, unaofanya kazi nzuri, kama watu wanachanga kuku,
bata, hii siyo dhambi. Wananchi wamekuwa wakarimu sana katika jambo
hili,” alisema Waziri Mkuu Pinda.
Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya (Chadema),
alitaka kufahamu ni kiasi gani cha fedha hutumika kwa kila wilaya kwa
ajili ya mbio za Mwenge, gharama za kuuwasha na kuuzima na faida
zinazopatikana.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Nkamia alisema Serikali hutenga fedha kulingana na mahitaji ya gharama halisi ya wakati husika.
Alitoa mfano wa mwaka 2012, Sh milioni 650 zilitengwa kwa ajili ya
kuadhimisha uzinduzi na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru; ambazo kati
ya hizo, Sh milioni 450 zilitumika na Wizara na Sh milioni 200
zilitumika na mkoa mwenyeji wa kilele cha mbio hizo.
Kuhusu faida, alitaja kuwa ni kuendelea kutunza historia na falsafa ya
ukombozi wa taifa, kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuendelea
kuenzi amani, mshikamano, upendo na zaidi kupambana na aina yoyote ile
ya kuwabagua Watanzania kwa rangi, dini au makabila yao.
Pia kuendelea kuhamasisha kushiriki katika shughuli za uzal- ishaji mali
na kujiletea maendeleo. Hata hivyo katika maswali ya nyongeza, Mbunge
wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), alisema Mwenge unaongeza ugumu wa
maisha kwa kuchangisha wananchi na kuwa viongozi wa mbio hizo mwaka huu
wanapita kupiga propaganda ya serikali mbili na kutaka mbio hizo
zifutwe.
Akijibu swali hilo, Nkamia alisisitiza kuwa Serikali haiko tayari
kusitisha mbio hizo, kwani wananchi wana imani nazo na zimesaidia
kudumisha umoja na amani.
Alisema Mwenge unatoa ujumbe mzuri kuliko unaotolewa na Ukawa. Mbali ya
Mnyika, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), alihoji sababu
za walimu kulazimishwa kuchangia mbio hizo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,Uratibu na Bunge, Wil- liam
Lukuvi alisema michango hiyo ni hiari na hakuna anayelazimish- wa
kuchangia, na kwamba hailipii mafuta ya Mwenge wala posho za
wakimbizaji.
Kwa upande wake, Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi (CCM), yeye
aliitaka Wizara ion- geze siku za kukimbizwa Mwenge wilayani Kishapu
kwani una manu- faa makubwa, na Wizara imeahidi kulifanyia kazi ombi
hilo huku ikipongeza hatua hiyo.
Baada ya hapo, Waziri Mkuu alitoa ufafanuzi zaidi, lakini baada ya
Kipindi cha Maswali na Majibu, wabunge wa upinzani walisi- mama tena na
kuomba Mwongozo kuhusu majibu hayo ya mawaziri.
Waliosimama ni Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (Chadema), Moses
Machali (NCCR- Mageuzi – Kasulu Mjini) na Susan Kiwanga (Viti Maalumu –
Chade- ma), wote wakieleza kuwa wananchi wanachangishwa, na baadhi yao
kusoma ujumbe waliotumiwa katika simu zao za mkononi. Naibu Spika Ndugai
alisema atatoa majibu ya miongozo hiyo ‘mbele ya safari.’

No comments:
Post a Comment