Mwanafunzi wa chuo afariki katika chumba cha boyfriend wake akijaribu kutoa mimba
Mwanafunzi wa Eden Hilling College aliyetajwa kwa jina la Atu Gabriel
amefariki akidaiwa kujaribu kutoa mimba kwa kunywa vidonge. Kwa mujibu
wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani (RPC), Orech Mtei,
katika kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, alisema Jumamosi April 26
mwili wa Atu ulikutwa katika chumba cha mwanaume aliyefahamika kwa jina
la Hafidhi ambaye anadaiwa kuwa mpenzi wake.
Kamanda Mtei ameeleza kuwa polisi walikuta mwili wa marehemu ukiwa karibu na vidonge alivyotumia huku akitokwa damu nyingi sehemu za siri na kwamba polisi wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa Hafidhi ambaye alidaiwa kukimbia baada ya tukio. “Ni kweli tukio hilo limetokea Jumamosi Aprili 26 mwaka huu eneo la Kwa Mfipa baada ya jeshi letu kutaarifiwa kuwepo kwa mwili huo na polisi walipofika na kufanya uchunguzi wake tulibaini marehemu alifariki dunia kaika jaribia la utoaji wa mimba…..hata hivyo mwili bado upo Hospitalini Tumbi kwa ajili ya uchunguzi zaidi,” alisema Kamanda Mtei.

“Baada ya tukio mtuhumiwa alikimbia na hadi sasa bado haijulikana alipo, jeshi letu linaendelea kumtafuta popote alipo na mara baada ya kumpata tutamuhoji na baadae atafikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua za kisheri,” alisema Mtei.
Secretary wa Eden Hilling College ambaye hakutaka jina lake litajwe
alieleza kuwa mwanafunzi huyo aliaga chuoni hapo siku ya Alhamisi kuwa
anakwenda katika hospitali ya Mwananyamala kumuuguza wifi yake na kwamba
wamesikitishwa sana na habari ya kifo cha mwanafunzi huyo. “Aliaga
vizuri tu siku ya Alhamisi kwamba anauguliwa na anakwenda kumuuguza wifi
yake aliyelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala lakini Jumamosi ndio
tukapokea taarifa za kifo chake! Hii inaonyesha huyu mwanafunzi
aliudanganya uongozi wa Chuo kitu ambacho hakikuwa sawa kabisa,”
Alisema.
Alisema hivi sasa uongozi wa Chuo unawasiliana na wazazi wake waliopo Makambaku kwa ajili ya kuja kuuchukuwa mwili wa marehemu.
Alisema hivi sasa uongozi wa Chuo unawasiliana na wazazi wake waliopo Makambaku kwa ajili ya kuja kuuchukuwa mwili wa marehemu.
No comments:
Post a Comment