MTUMISHI WA IDARA YA AFYA AKUTWA KAFIA GESTI
Mwili wa Marehemu Munuo ukitolewa katika Gesti hiyo
Mtumishi
wa idara ya Afya katika halmashauri ya mji wa Kahama, Mkoani Shinyanga,
Jeremiah Munuo (50) amekutwa amefariki dunia katika nyumba moja ya
kulala wageni mjini Kahama.
Taarifa kutoka jeshi la polisi
wilayani humo zimesema kwamba Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo
katika nyumba hiyo iitwayo KK Lodge iliyopo jirani na ofisi za
Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Taarifa zimesema watumishi wenzake
walikwenda kumuona leo majira ya saa 6 mchana baada ya simu yake kuita
bila kupokelewa kwa muda mrefu.
Jesh la polisi wilayani Kahama
limefika katika eneo la tukio na kumkuta marehemu Munuo ambaye alikuwa
na miezi 3 tu tangu ahamishiwe katika halmashauri hiyo akiwa na Fedha
taslimu shilingi 596,000 na simu nne za mkononi.
Mwili wa
marehemu Munuo umepelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti
cha hospitali ya wilaya hiyo na uchunguzi juu ya tukio hilo bado
unaendelea.

| Marehemu Munuo akiwa katika gesti hiyo alikokuwa amelala |
| mwili wa Marehemu Munuo baada ya kugeuzwa na kukaguliwa |
| Mwili wa Marehemu Munuoukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama |
No comments:
Post a Comment