Tuesday, 27 May 2014

Adam Kuambania alimtabiria Rachel Haule atajifungua mtoto wa kiume na amwite Kuambiana



Adam Kuambania alimtabiria Rachel Haule atajifungua mtoto wa kiume na amwite Kuambiana







Ikiwa ni wiki moja tangu afariki na kuzikwa kwenye makaburi ya
Kinondoni, msanii na muongozaji wa filamu, Adam Philip Kuambiana,
imebainika kuwa siku chache kabla ya kifo chake alimtabiria msanii
mwenzake ambaye kwa sasa ni marehemu Rachel Haule kuwa atajifungua mtoto
wa kiume na kumtaka ampe jina lake ‘Kuambiana’.




Akizungumza gazeti moja la burudani marehemu, Rachel 

Haule baada
kusikia kifo cha Kuambiana alisema kuwa alipongezwa na Adam na kumtaka
akijifungua kidume ampe jina lake. “Yaah kwanza alinipongeza kwa kuamua
kubeba mimba,pili akaniambia nikijifungua kidume nimuite jina lake,
tuombe Mungu nitakapojifungua tutajua,”
alisema marehemu Rachel enzi ya
uhai wake.
 
Rachel Haule alifariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali
ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam baada ya kujifungua mtoto kwa
operesheni na mtoto kufariki. 




Rachel sio msanii pekee aliyepoteza
maisha kutokana na uzazi. Msanii nyota wa muziki wa Taarab, Mariam
Khamis “Paka Mapepe” alifariki November mwaka 2012 katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili wakati akijifungua japo mwanae alipona.


No comments:

Post a Comment