Friday, 14 March 2014

WANAWAKE HAWA WAKIRI KUACHIA TIGO..!!



TIGO..!!





      

0

Mtafiti
Mwanasayansi Irine Mremi, kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa
Magonjwa ya Binaadamu nchini Tanzania (NIMR) ambaye aliwasilisha ripoti
hiyo kwa niaba ya watafiti wenzake wa NIMR. 



***
BAADHI ya wanawake kutoka katika Wilaya za  Kinondoni, Tanga, Makete na Siha, wamekiri kufanya ngono kinyume na maumbile.

Hayo
yalielezwa na Mtafiti Mwanasayansi Irine Mremi kutoka Taasisi ya Taifa
ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu nchini Tanzania (NIMR) wakati
akiwasilisha utafiti uliofanywa na watafiti wa NIMR juu ya ufanyaji
Ngono kinyume na maumbile katika kueneza maambukizi ya VVU/Ukimwi nchini
na kuwasilishwa mbele ya Wanahabari na Watafiti jijini Dar es Salaam
hivi karibuni.

Mremi
amesema wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya
ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi, Kuogopa kupata
Mimba, kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya
makabila.


Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka
15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi,
wafanyakazi, wahudumu bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani,
katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao
walihusishwa katika utafiti huo,” alisema Mtafiri Irine.

Aidha
alisema wakati wa utafiti huo wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa
walisema kuwa wanafanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile ambayo
ni sawa na 26.5%  huku 76.4% ya waliohojiwa walidai kufahamu njia hiyo
ya kufanya mapenzi.

Wilayani
Tanga ndio kumeonesha kukithiri kwa vitendo vya wanawake kufanya
mapenzi kinyume na maumbe na wanaume kuwafanyia wanawake kinyume na
maumbile ukilinganisha na Makete ambako bado kuna idadi ndogo.

Wanaume
waliohojiwa katika utafiti huo wamedai wao wanafanya kwa mtindo huo
kwaajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maambukizi ya
VVU/UKIMWI na wamekua wakitumia mafuta ya aina mbalimbali ilhali
matumizi ya mipira ikiwa ni hafifu kwani wakitumia mipira wamedai
kupunguza raha wanayo ipata.

Wanawake
pia wamedai baadhi ya tamaduni zao hasa maeneo ya Mwambao huko Tanga
msichana kuolewa na kukutwa usichana wake haupo (Bikira) ni aibu kwake
na wazazi hivyo hulazimika kufanya mapenzi kinyume na maumbile, huku
suala la Mimba nalo likichukua nafasi.

Watafiti
hao wamesema ufanyaji huo wa ngono kinyume na maumbile umekuwa
ukisababisha michubuko kirahisi na kuchangia maambukizi ya Ukimwi kwa
kasi tofauti na kutumia njia ya kawaida ya kujamiiana.

Aidha
imedaiwa kuwa wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na maumbile
wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao ya kushindwa
kuhimili kusukuma mtoto, jambo ambalo limekuwa likileta tabu kwa
wahudumu wa Afya hasa wakunga ambao ni wachache mahospitalini kutumia
muda mrefu kumhudumia mjazito mmoja huku wengine wakiendelea kuteseka
wodini wakati wa kujifungua.

Watafiti
hao wameshauri elimu zaidi ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi na njia
salama za kujamiiana kufundishwa mashuleni ili kuondoa dhana ya
kujamiiana kinyume na maumbile kuwa haiambukizi virusi vya Ukimwi.

  
Watafiti
walioshiriki katika utafiti huo ni pamoja na Akili kalinga, Elizabeth
 H Shayo,  Irene Mremi , Godlisten materu, Stella Kilima, Gibson
Kagaruki, Anjela  Shija, Judith Msovela, Dk. Leornad Mboera, Dk.Julius Massaga, Kesheni Senkoro na Basiliana Emid wote kutoka NIMR.

No comments:

Post a Comment