Mariam Ismail afunguka kuhusu madai ya kusagana na Irene Uwoya

Mastaa wa filamu nchini Mariam Ismail na Irene Uwoya wanadaiwa kuwa na
uhusiano wa kimapenzi(usagaji) na kudaiwa kuishi pamoja . Wiki
kadhaa nyuma muigizaji mmoja chipukizi anayekuja juu kwa kasi aliutonya
mtandao wa Swahiliworld kuwa Mastaa hao wajihusisha na penzi la jinsia moja.
"Mariam Ismail na Uwoya wanasagana tena wanaishi
pamoja kabisa, fuatilieni mtajua".
Baada ya habari hizo ilibidi
kuwatafuta mastaa hao,wa kwanza kutafutwa akiwa Irene Uwoya lakini
namba yake ya simu kwa takribani wiki 2 ilikuwa haipatikani na hata jana
alipotumiwa ujumbe kupitia namba yake nyingine hakujibu.
Baada ya hapo ilibidi kumtafuta Mariam Ismail ambaye wamecheza filamu
nyingi na Irene Uwoya kama vile Sobbing Sound, Omega Confusion, The
Return Of Omega na Apple.
Hata hivyo Mariam anayefanya vizuri katika
filamu alionekana kuwa busy na kuchelewa kujibu ujumbe wa madai ya
kusagana na Uwoya lakini jana star huyo aliyejipatia umaarufu kwa kuuvaa
vizuri uhusika katika filamu zake alitoa ushirikiano mzuri kwa kujibu
madai hayo akidai sio kweli ila yeye na Uwoya ni marafiki wa karibu sana
na wanasaidiana katika shida na raha ndiyo maana baadhi ya watu
wameshaanza kusema vibaya...
"Nadhani mimi ndio mtu wa kwanza
kupiga vita ujinga kama huo. Mimi ni mwanamke ambaye nimeumbwa
kikamilifu,sina kasoro yoyote ya kunifanya niwe na mwanamke
mwenzangu....
"Hao wanaofanya ujinga huo nadhani wana vijikasoro kwenye
mili yao.Irene Uwoya ni rafiki yangu sana tena urafiki wetu sio wa
leo wala kesho...
"Ni marafiki wa kushibana kabisa, nikoseapo huwa
ananikosoa na yeye akoseapo huwa namkosoa.Sometimes huwa tunagombana na
kupatana vitu ambavyo ni vya kawaida katika maisha." alisema Mariam ambaye hajawahi kukumbwa na skendo yoyote ile kabla ya hii.
Mariam ambaye kipaji chake cha filamu hujionyesha waziwazi alimalizia kwa kusema:
"Irene ananiheshimu
sana na mimi humuheshimu sana Irene, imefikia hatua ya mimi na yeye tukakaa
chini na kupanga tuishi wote kitu ambacho sioni tatizo na hilo.
"Ingekua
ni chumba kimoja hapo sawa, lakini ni nyumba kubwa yenye
kujitosheleza, kila mtu na room yake... Tunaishi kwa amani na kwa
kushirikiana. penye tatizo hulitatua wenyewe bila kumshirikisha mtu.
" Ukimya wetu na kupatana kwetu kusiwafanye watu kuanza kuhisi ujinga
juu yetu... Natumai ujumbe wangu utawafikia mashabiki wangu wote.
Asante. In god I trust."
>>Swahiliworld.
No comments:
Post a Comment