Friday, 24 January 2014

JAMANI DUNIA INA MAMBO: BABA AMLIPUA MWANAE MOTO, SOMA KISA HAPA



JAMANI DUNIA INA MAMBO: BABA AMLIPUA MWANAE MOTO, SOMA KISA HAPA







Stori: Francis godwin, Iringa
HUU ni
ukatili uliopitiliza! Wakati wanaharakati mbalimbali nchini wakiwemo
wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) wakipinga vikali vitendo vya
ukatili, baba wa kufikia, Musa Mdetela, mkazi wa mjini hapa anasakwa na
polisi kwa kosa la kuwachoma moto miguuni wanaye wa kambo.


Mdetela
anadaiwa kuwafanyia unyama huo watoto hao, Baraka anayesoma darasa la
kwanza na Mudi wa darasa la sita baada ya kuwatuhumu kuwa, waliiba
shilingi 10,000.

Wakizungumza na mwandishi wetu wakiwa katika
sura ya huzuni, watoto hao walisema baba huyo aliwatendea unyama huo
Januari 3, mwaka huu ambapo walijitetea kuwa walichukua ‘teni’ hiyo kwa ajili ya kununulia msosi baada ya mama yao kushindwa kuwaandalia chakula.


Hata
hivyo, Mudi alisema siku ya tukio mdogo wake (Baraka) aliingia
chumbani kwa baba yao na kuchukua kiasi hicho cha fedha kisha
wakashirikiana katika matumizi ambapo walinunua bagia na vitumbuia ili
wajipoze kwa njaa.

Wakizungumzia kuhusu baba yao mzazi (jina
tunalo), walisema aliwaacha mkoani hapa kwa muda mrefu na sasa anaishi
jijini Dar es Salaam hivyo wao wamebaki na baba mdogo huyo ambaye mara
kwa mara amekuwa akiwaadhibu vikali na kuwanyima chakula.


Kwa
masikitiko makubwa, walisema baada ya baba yao kurudi kutoka kwenye
shughuli zake na kubaini katika akiba yake teni haipo ndipo
alipowakamata na kuwafunga kamba na kuanza kuwatesa kwa kichapo ili
waseme mtu aliyekwapua pesa hiyo.

“Alitufunga kamba miguuni na
mikononi na kuanza kututesa kwa kutupiga. Alipoona hatusemi, akachukua
manailoni na kutufunga miguuni kisha akachukua kiberiti na mafuta ya taa
na kuwasha moto miguuni kwetu.

“Tulilia
sana, akaendelea kutupiga na moto ukiwaka. Wakati huo mama alikuwa
amekaa mlangoni akishangilia na kusema wapige sana mimi nimewachoka hao
watoto, heri wafe tu,” walisema watoto hao.

Imedaiwa kuwa baada
ya kutekeleza unyama huo, baba huyo aliwafungia ndani watoto hao na
kuwaambia wasitoke nje ndipo majirani walioshuhudia tukio hilo walipotoa
taarifa polisi katika kitengo cha dawati la jinsia wakalivalia njuga
swala hilo.

Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Iringa, Atupele
Mwambunda alizungumza na mwandishi wetu na kusema wamefanikiwa kumkamata
mama wa watoto hao, Watende Sanga huku mumewe, Mdetele aliyekimbia
akitafutwa kwa udi na uvumba ili kufikishwa kwenye mikono ya sheria.

Akiwa
katika ofisi za dawati la jinsia, mama wa watoto hao alidai wakati
baba yao mdogo akiwapa mbata watoto hao yeye hakujua kinachoendelea
japokuwa alipata taarifa ya kupotea kwa pesa.

Aliendelea kusema
kuwa, baada ya tukio hilo aliwanunulia dawa watoto hao ili kuwatibu
kinyemela pamoja na kuwaombea ruhusa shuleni.
Mwanamke huyo aliomba
kusamehewa kwa vile hakujua kama kushangilia wakati baba yao akiwapa
adhabu watoto hao ni kosa. Anaendelea kushikiliwa na polisi mkoani hapa.

KAMA ULIKUWA BADO HAUJAJIUNGA NAMI MOJA KWA MOJA ONLINE KWA MAPICHA ZAIDI

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment