Picha Na Info, Jamani Hii Ni Mara Ya Pili Nazushiwa "Sijafa" Mzee Small Asema.
Mzee Small aliyezaliwa mwaka 1955 kwa sasa anamiaka 58 ameshukuru sana sammisago.com kwa kuja kumtembelea na kumpa nafasi ya kusema machache kuhusu hali yake na kuwa
yuko hai na anaendelea vizuri.
Mzee Small alianza kwa kusema kuwa anaugua ugonjwa wa Kiharusi uliomfanya ashindwe kufanya kazi zake toka katikati ya mwaka jana, Mwezi May na alilazwa Hospitali ya muhimbili. Ugonjwa huu umeathiri zaidi mkono na mguu wake wa Kulia.
Mara ya kwanza Mzee Small alilazwa Amana kwa siku 3 na kuhamishiwa muhimbili kwa siku 7.Na baada ya hapo alirudi nyumbani na kuendelea na dawa.
Mke wa Small anasema amepokea taarifa za kuzushiwa kifo cha Mzee Small Mara Mbili toka Mzee ameanza kuumwa ila Uzushi wa mwaka huu ni mkubwa zaidi kwani amepokea simu zaidi ya 10 toka jana usiku mida ya saa sita mpaka Mzee alipomuambia azime simu.
Mzee Small amesema akipona bega na mguu wake atarudi tena kazini na kuanza kuigiza. Ni Baada ya wiki chache tu ana amini hivyo. Mzee anasema lazima arudi kwenye tasnia yake akipona na kupata mizuka.
Anawapa ushauri wasanii wa filamu na maigizo wapunguze uswahili na uzungu sana kwenye filamu na kuongeza ulimu na mafunzo kwa watu.
Mzee anashukuru sana sala na dua za WaTanzania na misaada tofauti anayo pokea kutoka kwa watu na anakaribisha mtu yoyote anayetaka kutoa chochote.
Filamu yake ya mwisho ilifanyika mwaka jana.




No comments:
Post a Comment