Wednesday, 27 November 2013

WASTARA NA BOND WAFUNGUKA BAADA YA KUDAIWA NI WAPENZI, ANTI LULU ANATAKA KUANDIKWA TU MAGAZETINI.


Juzi na jana kulikuwa na habari katika gazeti na mitandao
mingi kuwa Wastara na Bond Bin Suleiman ni wapenzi na
wamekuwa wakifanya siri sana huo uhusiano wao. Habari
ambazo zilinukuu chanzo kimoja zilieanda mbali zaidi
zikisema huenda Bond ana tabia ya kufanya mapenzi na
mwanamke kotekote kwani aliyekuwa mpenzi wake wa
zamani Lulu Semagongo(Anti Lulu) alidaiwa kuwahi
kukaririwa akisema kuwa anapenda sana kufanya mapenzi
kinyume na maumbile na hawezi kuacha tabia hiyo.
Baada ya habari hizo kusambaa ilibidi Swahiliworldplanet
kuwatafuta mastaa hao wawili na wa kwanza kupatikana
alikuwa ni Wastara na alikana kuwa katika penzi na Bond
ila alisema wanafanya kazi pamoja kwani kwasasa
wanashuti filamu mpya ya Bond inaitwa Uaminifu Dhaifu.
Aliongeza kwa kusema kuwa Bond ni kama kaka yake.
"sina mahusiano na Bond zaidi ya kikazi tu na zile picha
zote ambazo unaziona ni wakati tupo location tukiandaa
filamu yake inaitwa Uaminifu Dhaifu, huo ndiyo ukweli,
bora mume wangu angekuwepo haya yote yasingetokea"
Baada ya hapo ilibidi kumgeukia Bond ambaye yupo
location wakimalizia filamu hiyo na alipoelezewa hayo
alisema hana uhusiano wa kimapenzi na Wastara na picha
zinazodaiwa kuwa ni wapenzi ni za filamu mpya ambayo
tuliweka hata hapa SWP, alisema kuwa huyo Anti Lulu
anatafuta kuandikwa tu kwenye magazeti ndiyo maana
anatoa habari hizo zisizo za kweli ili kujipatia umaarufu
"Sio kweli ni picha za kazi tu ambazo hata wewe
nilikutumia magazeti yanazigeuza, Lulu achana nae
anatafuta kuandikwa, tulishachana kitambo wala hatuna
mawasiliano"
                                                               Anti Lulu....,,

No comments:

Post a Comment