Mwanamuziki wa P square, Peter Okoye ameoneshwa
kushangazwa na taarifa kwamba mwanamuziki wa bongo
fleva Naseeb Abdul alihudhuria harusi yake hivi karibuni
nchini Nigeria na kuhudhuriwa na mastaa mbali mbali
akiwenmo msukumba gozi wa Totenham Hotspurs
Adebayor.
Awali kupitia blogs mbali mbali kulisambaa taarifa kuwa
dimond alikua mwanamuziki pekee afrika mashariki
aliyealikwa katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na tajiri
nambari moja afrika, Aliko Dangote.
Blogs hizo zilikwenda mbali kwa kumpamba diamond kwa
vyeo vya ajabu ajabu ikiwemo Michael Jackson wa afrika
mashariki jambo ambalo lilisababisha wengi kumponda.
Akihojiwa na kituo cha EATV mara baada ya kuwasili jijini
Dar kwa ajili ya shoo iliyopigwa viwanja vya leaders club,
Okoye alishangazwa na taarifa za dimond kuhudhuria
katika harusi yake.
Okoye alikua akijibu swali aliloulizwaa na mtangazaji wa
kipindi cha HotMix Adrian Hilary kuhusu diamond
kuhudhuria harusi hiyo ambapo alionesha kushangazwa na
jina hilo na kuhoji Diamond ni nani?
Kushangaa huko kulimaanisha licha Diamond kujichezesha
mbele ya Okoye siku ya harusi yake lakini mwanamuziki
huyo hakua akijua aliyekua akimzungushia viuno vya
ngololo ni nani.
Picha ya diamond akikata viuno katika harusi hiyo-----!
Tuesday, 26 November 2013
P SQUARE WAMUUMBUA DIAMOND PLATNAM..!! HAYA NDIYO WALIYOSEMA.....!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment