Wednesday, 27 November 2013

AJIRA:Serikali yatangaza nafasi za kazi 2,748


Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania wenye sifa
na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 2,748 kwa
ajili ya waajiri mbalimbali Nchini.
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi
ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira
ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya waajiri
mbalimbali wa Ofisi za Umma.
Daudi alitaja nafasi za kazi zinazotangazwa kuwa ni Afisa
Uvuvi daraja la ii, Mvuvi msaidizi daraja la ii, Afisa Mifugo
msaidizi daraja la ii, Afisa mifugo daraja la ii, Mteknolijia
wa samaki daraja la ii, Daktari wa mifugo daraja la ii,Afisa
utafiti Mifugo daraja la ii, Daktari utafiti Mifugo daraja la ii,
Fundi sanifu Maabara Mifugo daraja la ii, Mkufunzi Mifugo
daraja ii, Mkufunzi wa Mifugo msaidizi na Daktari Mifugo.
Kada nyingine ni Mkufunzi daraja la ii, Mtekinolojia wa
Samaki msaidizi daraja la ii, uunda boti daraja ii, nafasi 2,
Dereva wa vivuko daraja la ii, msaidizi mifugo,afisa kilimo
daraja la ii, Afisa kilimo msaidizi daraja la ii, Mhandisi
kilimo daraja la ii, Fundi sanifu daraja la ii, Afisa utafiti
kilimo daraja la ii, Mkufunzi wa kilimo msaidizi, Afisa
kilimo msaidizi daraja la iii,Dereva daraja la ii, mlinzi,
Mhasibu mkuu daraja ii, Msanifu lugha mkuu iii na Afisa
vipimo.
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira nafasi hizo
za kazi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na
Maendeleo ya Mifugo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,
Chakula na Ushirika, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mlele,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Mpanda, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Nkasi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Sumbawanga na Mkurugenzi Manispaa ya Kinondoni.
Nafasi nyingine ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Chato, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Misenyi,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ngara, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Bukoba, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji
Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mkinga,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilindi, Mkurugenzi
Halmashauri ya Mji Korogwe, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Pangani, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Handeni, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Korogwe na
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Muheza.
Nafasi hizo pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Ulyankulu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uyui,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nzega, Mkurugenzi
Halmashauri ya Mji Nzega, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Igunga, Mkurugenzi Manispaa ya Tabora, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Ikungi, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Iramba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Manyoni,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Singida, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Itilima na Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Ushetu.
Waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Msalala, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kishapu,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bukombe, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Meatu, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Maswa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kahama,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bariadi, Mkurugenzi
Manispaa ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya
ya Nyasa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Namtumbo,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mbinga, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Manispaa ya
Songea, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Nyang`wale,
Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Misungwi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Ukerewe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Geita na
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Magu.
Nafasi hizo za kazi pia ni kwa aajili ya Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Tandahimba, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Newala, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Masasi, Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Masasi,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Gairo, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Mvomero, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Kilombero, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Ulanga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Morogoro,
Mkurugenzi Manispaa ya Morogoro, Mkurugenzi
Halmashauri ya Mji Tunduma, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Momba, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Mbarali, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ileje,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kyela, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Chunya, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Mbozi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Mbeya, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Rorya,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Serengeti, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Bunda, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Tarime, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Butiama, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Musoma,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ruangwa, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Nachingwea, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Lindi, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Mwanga na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Hai.
Katika nafasi hizo waajiri wengine ni Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Rombo, Mkurugenzi Halmashauri
Manispaa ya Moshi, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Kahama, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Uviza,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Monduli, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Babati, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Hanang, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Simanjiro, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Bagamoyo,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kisarawe, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Rufiji, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Iringa,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mufindi, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Makete, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Chamwino, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Mpwapwa,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Kongwa na Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Bahi,
Waajiri wengine katika nafasi hizo za kazi ni Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Chemba, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Kongwa, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Kilolo,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Makambako,
Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Ludewa, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Wanging`ombe, Mkurugenzi
Halmashauri Manispaa ya Kigoma, Mkurugenzi
Halmashauri Wilaya ya Kigoma, Mkurugenzi Halmashauri
Wilaya ya Kasulu, Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya
Kakonko, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu Tawala Mkoa
Pwani, Katibu Tawala Mkoa Dodoma, Katibu Tawala Mkoa
Iringa, Katibu Tawala Mkoa Kilimanjaro, Katibu Tawala
Mkoa Mtwara, Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Katibu
Tawala Mkoa Ruvuma, Katibu Tawala Mkoa Tabora, Katibu
Tawala Mkoa Kagera, Katibu Tawala Mkoa Dar es salaam,
Katibu Tawala Mkoa Rukwa, Katibu Tawala Mkoa Katavi,
Katibu Tawala Mkoa Njombe, Katibu Tawala Mkoa Njombe,
Katibu Tawala Mkoa Simiyu na Katibu Tawala Mkoa Geita.
Daudi amesema mwisho wa kupokea barua za maombi ya
kazi ni tarehe 10 Desemba, 2013. Aidha amewataka
waombaji wote wa fursa za ajira kutambua kwamba Kila
mwombaji kazi atapangwa katika kituo chochote cha kazi
bila kujali eneo au mahali alipoomba kutokana na mahitaji
ya mwajiri pamoja na idadi ya waombaji katika eneo
husika.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais-Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma. 27 Novemba, 2013...

No comments:

Post a Comment