Thursday, 12 March 2015
Mpango wa Kumuua Dr. Slaa: Mlinzi Wake Alipuka....Adai CHADEMA ni MAGAIDI......Asimulia Jinsi Alivyoteswa na Kupoteza Nguvu za Kiume
Siku chache kupita baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mabere Marando kufichua njama za Mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama hicho Wilbroad Slaa, bwana Khalid Kangezi kupanga mipango ya kumuua katibu huyo huku akishirikiana na Vigogo wa Chama Mapinduzi CCM pamoja na Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Kinondoni,naye Mlinzi huyo ameibuka na kufichua siri nzito ndani ya Chama hicho kikuu cha upinzani nchini..Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kangezi amesema siku ya kifo cha marehemu Kapteni John Komba alikuwa akitokea nyumbani kwake Mwenge akielekea kazini nyumbani kwa Dk. Slaa ambapo baada ya kufika getini aliambiwa na mlinzi wa geti hilo kuwa haruhusiwi kuingia ndani na alipouliza sababu alijibiwa kuwa taarifa imetoka kwa mke wa Dk. Slaa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment