Mwanamuziki
nguli wa kike hapa Tanzania Lady JayDee ambaye kwa sasa anafanya poa na
wimbo wake wa Forever amefunguka na kuonyesha kukerwa na kitendo cha
baadhi ya mashabiki wake wa Instagram ambao walimuelewa vibaya baada ya
kupost picha jana
Msanii Lady Jaydee na Mbunge viti Maalumu (CCM) Katherine Magige.
na
kusema kuwa tumbo lake limevimba baada ya kupata msosi wa maana na
mzuri,Mashabiki hao wengi wao walitafsiri kuwa Mwanadada huyo kwa sasa
ni Mjamzito baada ya kuona picha ile na maneno ya Jide yaliyosomeka kama
Tumbo limevimba sababu ya sahani.
Lady
JayDee ilibidi aifute ile post aliyopost na kupokelewa tofauti na
baadhi ya mashabiki wake na kisha aliandika maneno haya kuonyesha
kutopendezwa kabisaa na baadhi ya mashabiki walioshadadia kuwa
ametundikwa mimba,huku wengine wakionyesha kumnyanyapa.
"Imebidi
nifute post Ili nielezee upya.Hivi watu hamuelewi kiswahili au ni nini
??? Nimesema tumbo limevimba sababu ya sahani,nikimaanisha mlo na nili
post nakula hapo awali Sasa hayo maneno mengine yanatokea wapi? Au niwe
naandika kichina? Kwani mliambiwa nitazaa Rais atakaewatoa katika shida
zote mpaka mnishikilie mimba mimba..Hebu niacheni basi khaaa Nisiishi
Kisa mimba? Aisee mnaboa sana. Basi niueni Kisa sijazaa Ili niwaondolee
kero kabisa."
Mashabiki
wa Lady Jaydee wameonyesha kumtia moyo mwanadada huyo baada ya
mashabiki wengine kuanza kuandika vitu vibaya huku wengine wakimdhihaki
kuwa hawezi kupata ujauzito na kumwita majina ya ajabu ajabu mwanamuziki
huyo.
"Mwangaza84:
Fanya yako mama, binadamu hawakosi la kuongea.Kwani mtu bila mimba
maisha hayaendi? Stupid pipo always think about t stupid things.youre
the best and you do best music ever in Tanzania hatotokea kama wewe. Big
up sisister"
"Ilotha_boniphace:
"Hayo nimapenzi ya mungu namungu ndio amepanga usijali Jide huyu huyu
mungu alie kupa uhai ndo atakupa haja yamoyo wako nahayo nimaneno ya
binadamu yanapita but ya mungu kamwe hayapiti so jipe moyo my sister"
"Martha_mollel:
Hata wao wanavizazi kama wanataka watoto wakazae wao, wakuache, binadam
bwana mnaboa mimba mimba si mzae na nyie, mafi yenu..."
"Jokofu2:
Kila kitu ni majaliwa ya allah kuongelea jambo usilolijua nimpango wa
kibinadamu, hivo puuza na usiumize kichwa dada jide."
No comments:
Post a Comment