Tuesday, 10 March 2015

Flora Mbasha Atoa Ushahidi wake Kwa Siri Kuhusu Kesi ya Ubakaji Inayomkabili Mumewe, Emmanuel Mbasha


Kesi ya kudaiwa kumbaka shemeji yake inayomkabili mfanyabiashara na mwimba Injili Bongo, Emmanuel Mbasha imeendelea kuunguruma leo katika Mahakama ya Ilala jijini Dar ambapo mkewe Flora alifika na kutoa ushahidi kwa siri.Kesi hiyo ilianza kuunguruma kwenye ofisi ya hakimu (Chamber), mishale ya saa 5 hadi saa 8 mchana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama wa Wilaya ya Ilala, Flora Mjaya ambapo shahidi namba tatu, Flora aliitwa kutoa ushahidi wake. Kesi hiyo inaendeshwa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Nassoro Katuga na imeahirishwa hadi Aprili 16, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment