Thursday, 12 March 2015

Bongo DSM: Monalisa Ndani-Dude



Bongo DSM: Monalisa Ndani-Dude
  • Bongo DSM: Monalisa Ndani-Dude 1
Mwigizaji na mwongozaji wa filamu, Kulwa Kikumba  ‘Dude’ ambae ni mmiliki na mwigizaji igizo la Bongo Dar-es-salaam ambalo  hurushwa kwenye runinga, amemtaja mwigizaji Yvonne-Sheryl Ngatikwa 'Monalisa’ kuwa ni moja kati ya wakali watakaoshiriki kwenye kipindi hicho kwa msimu huu.
Kitendo cha kumuongeza Monalisa kwenye timu ya Bongo DSM kimewafurahisha wengi na kuongeza hamasa kubwa miongoni mwa wapenzi wengi wa kipindi hicho ambacho kilijizolea umaarufu mkubwa miaka ya zaidi ya mitatu iliyopita.
Pamoja na Monalisa hapo awali Dude alimtaja  Haji Adam ‘Baba Haji’ kuwa ni moja kati ya waigizaji wakali watakaoshiriki kwenye Bongo DSM ya  msimu huu.
Dude pia alisisitiza kuwa kipindi hicho kitaanza kuonekana hivi punde kwenye runiga zetu.
Kila la kheri wana Bongo DSM.

No comments:

Post a Comment