WAKATI
serikali kupita Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ikisema
itakifuta cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu,
taarifa zinasema kwamba hawezi tena kuendelea na taji hilo.
Inaelezwa
kwamba uamuzi umekwisha kufanyika wa kumvua Sitti taji hilo alilovikwa
katika mazingira tata, uamuzi unaotarajiwa kutangazwa wakati wowote
kuanzia sasa.
Hata
hivyo, haijafahamika kama hatua hiyo itachukuliwa na Baraza la Sanaa
Tanzania (BASATA) ama Sitti mwenyewe baada ya kubainika kwamba taji hilo
linazidi kuiweka pabaya familia ya Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu,
ambaye ni baba yake.
Uchunguzi
wa mwandishi wa habari hizi umebaini kwamba hata hatua ya awali ya
kuwania taji hilo ilichukuliwa na Sitti na baadhi ya wanafamilia bila
kushirikishwa kwa Mbunge Mtemvu, jambo ambalo lilimsononesha awali
katika ushiriki wa Miss Temeke.
Imeelezwa
kwamba Mbunge Mtemvu amekerwa na hali inayoendelea ikiwa ni pamoja na
kuwapo utata wa cheti cha kuzaliwa cha mwanae Sitti, pamoja na kuwa
anawajibika kisheria kwa anayoyafanya kutokana na kufikia umri wa zaidi
ya miaka 18.
Kwa
upande wake, RITA imesema inaweza kukifuta cheti kilichotolewa Temeke
na kuchukua hatua stahiki ikibainika kwamba alitoa taarifa za uongo
wakati wa kuwasilisha maombi ya kukupata cheti hicho.
Mtendaji
Mkuu wa RITA, Philip Saliboko,amesema kwamba kwa sasa wanakamilisha
uchunguzi wa kina kuhusiana na cheti hicho, baada ya kuibuka utata wa
taarifa za kuwapo vyeti viwili vinavyotofautiana mwaka wa kuzaliwa.
Baada
ya kuibuka kwa utata huo, RITA ilianza upekuzi maalumu wa nyaraka
alizowasilisha Sitti katika ofisi za RITA Temeke ili kubaini kwanza
uhalali wa cheti, kabla ya kutafuta ukweli wa taarifa zilizowasilishwa
chini ya kiapo.
Kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Sura ya 108 Toleo la 2002), ni kosa la jinai kutoa…
via>>Fikra Pevu

No comments:
Post a Comment