Naibu Waziri wa zamani wa Afya na mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Lucy Nkya, amerushiana risasi za moto na mwanae wa kumzaa, Jonas Nkya ndani ya ofisi zao mkoani Morogoro
Kufuatia taarifa zilizozagaa mjini morogoro na kuripotiwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mbunge wa jimbo la morogoro kusini, Dk Lucy Nkya na mwanaye Jonas Nkya ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa kupitia vijana, kurushiana risasi kwenye ofisi yao binafsi ya faraja trust fund, watu hao wawili wamekanusha madai hayo na kudai yameleta athari kubwa katika familia yao.
Awali
taarifa zilizojitokeza na baadaye kurushwa kwenye mitandao mbalimbali
ya kijamii, ilikuwa ni mama huyo aliyewahi kuwa naibu waziri wa afya, na
mwanaye ambaye ni mjumbe wa NEC akiwakilisha vijana, kurushiana risasi
kwa kugombea nyumba iliyotaka kuuzwa jijini Dar es salaam, hali
iliyofanya ITV kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Leonard
Paulo ambaye kwa njia ya simu amekiri tukio la mlio wa risasi kujitokeza
katika ofisi za faraja, lakini mazingira yake hawezi kuzungumzia hadi
arudi ofisini, kwavile alikuwa safarini.
Hata
hivyo Jonas Nkya alipopatikana amekanusha madai hayo na kwamba
kilichojitokeza ni kuanguka kwa bastola yake iliyokuwa kiunoni, baada ya
kwenda ofisi za faraja kubadilisha gari kwaajili ya kwenda shamba,
ambapo ilijifyetua risasi mbili na kutoa mlio uliosababisha baadhi ya
watu kusogea eneo hilo na kwamba kama kungekuwa na ugomvi wa kifamilia,
ungefanyika nyumbani kwao ambapo yupo kwa sasa, akimsaidia mama yake
kumuuguza baba yake Prof Nkya,ambaye amepooza, madai ambayo yameungwa
mkono na mama yake mzazi ambaye naye amehojiwa katika ofisi za faraja,
baada ya kukutwa akiendelea na majukumu yake.
No comments:
Post a Comment