Msala
huo wa aina yake ambao ulivuta umati mkubwa ulijiri wikiendi iliyopita
maeneo ya Makumbusho jijini Dar baada ya kijana huyo kuwekewa mtego na
kukutwa na mke wa mtu akimsomesha.
Adabu
ishike mkondo wake! Njemba aliyetajwa kwa jina moja la Jose amejikuta
akichezea kichapo ‘hevi’ kilichomsababishia kuvunjika pua kwa tuhuma ya
ukuwadi wa mke wa mtu.
Kwa mujibu wa jamaa waliomwekea mtego
Jose (wa kwanza kulia pichani juu), jamaa huyo amekuwa sugu mtaani hapo
kiasi cha kuwakera baadhi ya vijana wenye wapenzi na wake zao.Jose
alishuhudiwa akila kichapo kutoka kwa vijana wasiotaka kufuata sheria
bila shurti hadi akatiririkwa damu chapachapa puani baada ya kuvunjika
pua.
“Haiwezekani awe anawakuwadia wake zetu kwa wanaume wengine, leo
tulipanga tumtoboe hata jicho moja ili liwe fundisho kwake na wengine
wenye tabia kama za Jose,” alisema mmoja wa vijana waliokuwa wakimsulubu
jamaa huyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema, mwanaume aliyemwekea
mtego Jose ambaye aliomba hifadhi ya jina gazetini alisema kwamba,
waliamua kumpa mkong’oto kijana huyo baada ya kuchoshwa na vitendo vyake
hivyo.
Alisema hata mkewe alishamuonya juu ya mazoea na Jose na kumweleza kuwa
akimkuta tu na kijana huyo lazima atampa talaka jambo ambalo lipo kwenye
‘prosesi’.
Kwa upande wake Jose alishindwa kusema lolote huku akisikilizia maumivu
ya kipigo hadi alipoondolewa eneo la tukio na wasamaria wema
No comments:
Post a Comment